The chat will start when you send the first message.
1Bwana, liinamishe sikio lako, uniitikie! Kwani mimi ni mnyonge, hata mkiwa.
2Ilinde roho yangu! Kwani mimi ninakucha. Wewe Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako aliyekuegemea![#Sh. 18:21-27.]
3Wewe Bwana, nihurumie! Kwani ninakulilia mchana kutwa.[#Sh. 6:3.]
4Roho ya mtumishi wako ifurahishe! Kwani ninakuinulia roho yangu, ikutazamie, Bwana.
5Kwani wewe Bwana u mwema, unapenda kuondoa makosa, upole wako ni mwingi kwao wakuliliao.[#Sh. 86:15.]
6Sikia, Bwana, ninayokuomba! Sauti ya malalamiko yangu itegee masikio!
7Siku, ninaposongeka, ninakuita, kwani unaniitikia.[#Sh. 50:15.]
8Miongoni mwa miungu hayumo aliye kama wewe, Bwana, hayumo awezaye kufanya matendo kama yako.[#Sh. 71:19.]
9Wamizimu wote, uliowafanya, watakuja, wakuangukie, nalo Jina lako, Bwana, watalitukuza.
10Kwani wewe u mkubwa, unafanya mataajabu, aliye Mungu niwewe peke yako.
11Nifundishe, Bwana, njia yako, niendelee na kweli yako! Ushike moyo wangu, upende moja tu: kuliogopa Jina lako![#Sh. 27:11.]
12Nitakushukuru, Bwana Mungu wangu, kwa moyo wote na kulitukuza Jina lako kale na kale.
13Kwani upole wako, ulionitolea umekuwa mkubwa, ukaiopoa roho yangu kuzimuni chini ya nchi.
14Mungu, wako wenye majivuno walioniinukia, ni kundi zima la wakorofi, wanaitafuta roho yangu, lakini wewe hawakutaki kuwa machoni pao.
15Nawe wewe Bwana u Mungu mwenye huruma na utu, tena u mwenye uvumilivu na upole na welekevu mwingi.[#2 Mose 34:6.]
16Rudi upande wangu na kunihurumia! Mpe mtumishi wako nguvu ya kwako! Mwana wa mjakazi wako umwokoe![#Sh. 116:16.]
17Nifanyizie kielekezo kinipatiacho mema, wachukivu wangu wakione, waingiwe na soni, kwa kuwa wewe Bwana umenisaidia, ukanituliza moyo.