The chat will start when you send the first message.
1Wimbo wa wana wa Kora, waliomtungia mwimbishaji, auimbishe kama wimbo wa kwamba: Ugonjwa huinamisha. Fundisho la Hemani aliye wa ukoo wa Ezera.[#1 Mambo 6:33; 25:1.]
2Bwana Mungu uniokoaye, mchana ninakulilia, usiku nao sikuachi,
3sharti yafike kwako malalamiko yangu. Liinamishe sikio lako, nikikupigia kelele!
4Kwani roho yangu imeshiba kwa kuona mabaya, uzima wangu umekwisha, kuzimu kumenijia karibu.
5Ninahesabiwa kuwa mwenzao washukao shimoni, nimegeuka kuwa kama mtu asiye na nguvu hata kidogo.
6Kilalo changu kiko kwao waliokwisha kufa, ninafanana nao waliouawa vitani walalao makaburini; huwakumbuki tena waliokwisha kutengwa, watoke mkononi mwako.
7Umenilaza shimoni ndani ya nchi kwenye giza lililomo humo kuzimuni.
8Makali yako yamenilemea, mawimbi yako yote yamenikwelea.[#Sh. 42:8.]
9Wenyeji wangu umewahamisha, nisiwaone, ukaniweka kuwa tapisho kwao hao; hivyo, nilivyofungwa, sitaweza kutoka.[#Sh. 31:12; 38:12; 88:19.]
10Macho yangu yamefifizwa kwa kuumia, ninakulilia, Bwana, mchana kutwa na kukunyoshea wewe mikono yangu.
11Je? Utafanya kioja kwenye wafu? Au vivuli vitainuka, vikushukuru?[#Sh. 6:6.]
12Je? Mambo ya upole wako yanasimuliwa makaburini? Au mambo ya welekevu wako yanasimuliwa kuzimuni?
13Je? Vioja vyako vinatambulikana kwenye giza? Au wongofu wako katika nchi ikaayo walioyasahau yote?
14Lakini mimi ninakupigia kelele wewe, Bwana, malalamiko yangu hufika kwako asubuhi na mapema.
15Mbona unaitupa roho yangu, wewe Bwana? Mbona unauficha uso wako, nisiuone?
16Mimi ni mnyonge na mwele toka utoto wangu, nikayavumilia mastuko yako, kisha nikazimia.
17Makali yako yenye moto yamenikwelea, matetemeko yako yakanizimisha roho.
18Yalinizunguka siku zote kama maji, yakanizinga na kunisonga pawapo pote.
19Wenzangu wapendwa umewahamisha, nisiwaone tena; wenyeji wangu waliosalia ni giza tupu.[#Sh. 88:9.]