Mashangilio 93

Mashangilio 93

Utukufu wake Mungu.

1*Bwana ni mfalme, huvaa yenye urembo; kweli Bwana huvaa, nayo nguvu ndiyo, aliyojifunga kiunoni. Hivyo ndivyo, alivyoishikiza nchi, isije kuyumbayumba.[#Sh. 96:10; 97:1; 99:1; 2 Mose 15:18.]

2Kiti chake cha kifalme kimeshikizwa na nguvu tangu mwanzo, tangu kale na kale wewe upo.

3Bwana, huzivumisha sauti zao mito mikubwa, kweli mito mikubwa huzivumisha sauti zao, huvivumisha vishindo vyao hiyo mito mikubwa.

4Lakini nguvu za mavumi ya hayo mafuriko ya maji yaliyo mengi, hata nguvu za mawimbi ya bahari yaumukayo zinapitwa na nguvu zake Bwana atukukaye. Mashuhuda yako hutegemeka sana,

5pambo liipasalo Nyumba yako, Bwana, ndio utakatifu, nao utakuwako siku zote zitakazokuwa.*[#Sh. 19:8-11.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania