The chat will start when you send the first message.
1Njoni, tumpigie vigelegele yeye Bwana! Aliye mwamba wa wokovu wetu na tumshangilie![#Sh. 81:1.]
2Na tumtokee usoni pake na kumshukuru! Na tumshangilie na kumwimbia!
3Kwani Bwana ndiye Mungu aliye mkuu, ni mfalme mkuu kuliko miungu yote.[#Sh. 96:4.]
4Kwani mkononi mwake vimo vilivyomo ndani ya nchi, vileleni kwa milima nako ndiko kwake.
5Bahari ni yake, maana ndiye aliyeifanya, mikono yake iliziumba nazo hizo nchi kavu.
6Njoni, tumtambikie na kumwangukia! Na tupige magoti mbele yake Bwana aliyetufanya!
7Kwani yeye ni Mungu wetu, nasi watu wake, hutuchunga kwa kuwa kondoo waliomo mkononi mwake.[#Sh. 100:3; Yoh. 10:27-28; Ebr. 3:7; 4:7.]
8Leo mtakapoisikia sauti yake, msiishupaze mioyo yenu, kama vilivyokuwa kule Meriba au Masa, mlipokuwa kule nyikani.[#Ebr. 3:7-8; 4:7.]
9Ndipo, baba zenu waliponijaribu na kunipima, tena walikuwa wameyaona matendo yangu.[#2 Mose 17:2-7.]
10Nikachafuliwa moyo miaka arobaini nao wa kizazi hicho, nikasema: Wao ndio watu walioipoteza mioyo yao, nao ndio waliokataa kuzitambua njia zangu.
11Kwa hiyo nilijiapia kwa makali yangu: Hawataingia kamwe kwenye kituo changu![#4 Mose 14:22-23; Ebr. 4:3.]