The chat will start when you send the first message.
1Mwimbieni Bwana wimbo mpya! Kwani hufanya mataajabu. Mkono wake wa kuume humpatia kushinda. maana huo mkono wake ni wenye utakatifu.[#Sh. 33:3.]
2Bwana huujulisha wokovu wake, machoni pao wamizimu huufunua wongofu wake.
3Huukumbuka upole na welekevu wake, aliouagia mlango wa Isiraeli, mapeo yote ya nchi yameuona wokovu wa Mungu wetu.[#Yes. 52:10.]
4Mpigieni Bwana shangwe, nchi zote! Pazeni sauti! Shangilieni na kumwimbia!
5Mwimbieni Bwana na kupiga mazeze, mazeze yakizifuata sauti za nyimbo!
6Pigeni mabaragumu yenye kulia sana mkishangilia mbele yake bwana, ya kuwa ni mfalme![#4 Mose 23:21.]
7Bahari na ivume nayo yote yaliyomo! Hata nchi pamoja nao wakaao humo![#Sh. 96:11-13.]
8Mito mikubwa na iitikie na milima pamoja, yote na ishangilie!
9Bwana atakapokuja ataihukumu nchi, atauhukumu ulimwengu kwa wongofu nayo makabila ya watu kwa unyofu.*