The chat will start when you send the first message.
1Bwana ni mfalme, kwa hiyo makabila ya watu hutetemeka. Yeye anakaa juu ya Makerubi, lakini nchi inayumbayumba.[#Sh. 80:2; 93:1.]
2Bwana ni mkuu mle Sioni, anayapita makabila yote ya watu kwa kutukuka.
3Na walishukuru Jina lako kubwa lililo la kuogopesha; aliye mtakatifu ndiye yeye.
4Nguvu za mfalme huyu ni kupenda maamuzi yaliyo sawa. Wewe ndiwe uliyetoa unyofu wa kuyashikiza, nawe ndiwe uliyeamua kwa Yakobo maamuzi yaongokayo.[#Yes. 9:7.]
5Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu! Hapo, anapoiwekea miguu yake, mwangukieni! Aliye mtakatifu ndiye yeye.[#1 Mambo 28:2.]
6Mose na Haroni walikuwa miongoni mwao watambikaji wake, Samueli alikuwa miongoni mwao waliolililia Jina lake.[#Yer. 15:1.]
7Alisema nao akiwa amejificha katika wingu lililokuwa kama nguzo, wao wakayashika maneno, aliyowashuhudia, hata maagizo, aliyowapa.
8Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu. uliwaitikia kwa kuwa Mungu wao aondoaye makosa, tena kwa ajili ya matendo yao ukawalipiza.
9Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu! Mwangukieni mlimani kwenye utakatifu wake! Kwani Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.