The chat will start when you send the first message.
1Sasa tusemeje? Tufulize kukosa, magawio nayo yafurike?[#Rom. 3:5,8.]
2La, sivyo! Sisi tulioyafia makosa tutawezaje kuishi nayo tena?
3*Au hamjui, ya kuwa sote tuliobatiziwa, tuwe wake Kristo Yesu, tulibatiziwa, tufe naye?[#Gal. 3:27; Kol. 2:12; 1 Petr. 3:21.]
4Hivyo tulizikwa pamoja naye tulipobatiziwa, tufe naye, ni kwamba: Kama Kristo alivyofufuliwa katika wafu kwa nguvu ya utukufu wa Baba, vivyo nasi sharti tupate upya wa maisha, tuendelee nao.
5Kwani tulivyounganika naye tulipokufa, kama alivyokufa, vivyo tutafufuka nasi, kama alivyofufuka yeye.[#Fil. 3:10-11.]
6Kwani tunalitambua neno hili: mtu wetu wa kale amewambwa msalabani pamoja naye, miili yetu yeye kukosa ipate kukomeshwa, sisi tusiyatumikie tena makosa kama watumwa.[#Gal. 5:24; Ef. 4:22.]
7Kwani aliyekufa amekwisha kupata wongofu kwa kuondolewa kwenye makosa.
8Nasi kama tumekufa pamoja na Kristo, tunalitegemea la kwamba: Tutaishi pamoja naye.[#Rom. 6:4.]
9Kwani twajua, ya kuwa Kristo hafi tena kwa hivyo, alivyofufuliwa katika wafu, kifo hakina ufalme tena wa kumshika.
10Kwani hivyo, alivyokufa, aliyafia makosa na kuyashinda papo hapo; lakini hivyo, anavyoishi, anaishi, amtumikie Mungu.[#Ebr. 9:26-28.]
11Nanyi jiwazieni hivyo: makosa mmekwisha kuyafia, lakini sasa mnaishi, mmtumikie Mungu katika Kristo Yesu!*[#2 Kor. 5:15; 1 Petr. 2:24.]
12Kwa hiyo ukosaji usishike ufalme katika miili yenu yenye kufa, mzitii tamaa zao![#1 Mose 4:7.]
13Wala msivitoe viungo vyenu, viwe mata ya upotovu ya kuyatumikia makosa! Ila mjitoe wenyewe kumtumikia Mungu kwa hivyo, mnavyoishi, tena mlikuwa mmekwisha kufa! Navyo viungo vyenu mvitoe, viwe mata ya wongofu ya kumtumikia Mungu![#Rom. 12:1.]
14Kwani ukosaji hautashika ufalme, uwatawale, maana nguvu yenu siyo ya Maonyo, ila ya upole.[#1 Yoh. 3:6.]
15Basi, inakuwaje? Tukose vivyo hivyo, kwa sababu nguvu yetu siyo ya Maonyo, ila ya upole? La sivyo![#Rom. 5:17,21.]
16Hamjui, vilivyo? Ni hivi: mnapojitoa wenyewe kumtumikia mtu kitumwa na kumtii, basi, mmekwisha kuwa watumwa wake yeye, mnayemtii. Ikiwa ni wa ukosaji, mnakwenda kufa; ikiwa ni wa wito, mnakwenda kupata wongofu.[#Yoh. 8:34.]
17Lakini Mungu atolewe shukrani, kwa sababu ninyi mliokuwa watumwa wa ukosaji mmegeuzwa mioyo, mkaja kuyatii mafundisho, kama mlivyoyapata!
18Napo hapo, mlipokombolewa katika utumwa wa ukosaji, mmegeuka kuwa watumwa wa wongofu.[#Yoh. 8:32.]
19*Nasema kimtu kwa ajili ya unyonge wa miili yenu: Kama mlivyovitoa viungo vyenu kuutumikia kitumwa uchafu na upotovu, mkajifikisha penye kupotolewa, vivyo hivyo vitoeni sasa viungo vyenu kuutumikia kitumwa wongofu, mjifikishe penye kutakaswa!
20Kwani mlipokuwa watumwa wa ukosaji, siku zile mlikuwa hamna wongofu hata kidogo.
21Basi, siku zile mlikuwa na mapato gani? Sasa hivi mnayaonea soni, kwani mwisho wao ni kufa.[#Rom. 8:6,13; Ez. 16:61,63.]
22Lakini sasa kwa kuwa mmekwisha kukombolewa katika utumwa wa ukosaji, mkawa watumwa wake Mungu, mnayo mapato yenu kwa kujifikisha penye kutakaswa, tena mwisho mtapata uzima wa kale na kale.[#1 Petr. 1:9.]
23Kwani mshahara wa ukosaji ni kufa; lakini gawio, Mungu analotupa katika Bwana wetu Kristo Yesu, ni uzuma wa kale na kale.[#Rom. 5:12; 8:6.]