The chat will start when you send the first message.
1Nilipolala usiku nilimtafuta yeye, roho yangu inayempenda;
2Na niinuke, nizunguke mjini,
roho yangu inayempenda nimtafute barabarani na viwanjani;
3Walinzi wazungukao mjini waliponiona,
nikawauliza: Mmemwona yeye, roho yangu inayempenda?
4Nilipokwisha kuwapita kwenda mbele kidogo,
ndipo, nilipomwona yeye, roho yangu inayempenda.
Nikamshika, nisimwachie tena,
mpaka nikamwingiza nyumbani mwa mama yangu,
5“Nawaapisha ninyi, wanawake wa Yerusalemu,
nikiwataja paa na kulungu wake walioko porini,
msimwamshe, wala msimhangaishe yeye ninayempenda,
ila mwacheni tu, mpaka atakapopendezwa wenyewe!”
6Ni nani huyo apandaye kutoka nyikani?
Anafanana kuwa kama wingu la moshi lililo kama nguzo,
ni manemane na uvumba aliyovukiziwa
na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi yanukayo vizuri.
7Tazameni! Kiko kiti, ni cha kifalme cha Salomo!
Wanguvu sitini wanakizunguka, ndio wanguvu wa Waisiraeli.
8Wao wote wanashika panga, ni mafundi wa vita,
kila mmoja anao upanga wake kiunoni pake
wa kukingia mastusho ya usiku.
9Kiti hicho mfalme Salomo alijitengenezea kwa miti ya Libanoni,
10miguu yake aliifanya kwa fedha, maegemeo ni ya dhahabu,
pa kukalia ni nguo nyekundu za kifalme.
Hapo kati yako marembo mazuri mno yaliyoshonwa
na wanawake wa Yerusalemu ya kumpendeza mfalme.
11Tokeni, wanawake wa Yerusalemu, mmtazame mfalme Salomo!
Amevika kilemba, mama yake alichomfunga siku ya ndoa yake,
maana ndiyo siku, moyo wake uliyoifurahia.