The chat will start when you send the first message.
2Mpendwa wangu ameshuka kwenda bustanini pake,
kutembea bustanini penye matuta ya manukato,
3Mimi ni wake mpendwa wangu, naye mpendwa wangu ni wangu mimi;
4“Kweli u mzuri kama Tirsa, unapendeza kama Yerusalemu,
tena unaogopesha, mpenzi wangu, kama vikosi vyenye bendera.
5Yageuze macho yako, yasinitazame, kwani hunitatanisha;
nywele zako zinafanana na kundi la mbuzi
walalao upande wa kushukia wa milimani kwa Gileadi.
6Meno yako ni kama kundi la kondoo wanaotoka kuogeshwa,
kwao hakuna hata mmoja aliye peke yake.
7Shavu lako huonekana mtandioni mwako
kuwa kama komamanga ipevukayo sana.
8Wako wanawake wa kifalme sitini na masuria themanini,
tena wako wanawali wasiohesabika.
9Lakini yuko mmoja tu aliye hua wangu na mwenzangu atakataye,
ni mwana wa pekee wa mama yake, aliyemzaa humpenda sana;
wanawali wenzake wakimwona humwazia kuwa mwenye shangwe,
nao wanawake wa kifalme na masuria humtukuza.”
10“Nani huyu mwanamke aonekaye kama mapambuzuko?
Ni mzuri kama mwezi, anang'aa kama jua,
anaogopesha kama vikosi vilivo vyenye bendera.”
11Nilishuka kwenda bustanini penye milozi,
nijifurahishe kwa kuyaona machipukizi mapya yaliyoko bondeni;
tena nilitaka kuitazama mizabibu, kama imechanua,
nayo mikomamanga, kama imepata maua.
12Nilipokuwa siviangalii, roho yangu ikanipeleka,
ikaniweka penye magari, nayo yalikuwa ya wakuu wa kwetu.