Wimbo mkuu 7

Wimbo mkuu 7

Maongezi ya mpendwa mume na mpenzi mke.

1Miguu yako yenye mitalawanda ni mizuri mno, binti mkuu!

Viuno vyako vinaviringana kama mapambo ya shingoni

yaliyotengenezwa na mikono ya mtu aliye fundi kweli.

2Kitovu chako ni kama chano kilichoviringana,

kisichokosa mvinyo iliyotiwa viungo vizuri;

tumbo lako ni kama chungu ya ngano iliyozingwa na nyinyoro.

3Maziwa yako mawili hufanana na vitoto viwili vya kulungu,

4Shingo yako ni kama mnara wa meno ya tembo,

macho yako ni kama viziwa vya kuko Hesiboni,

vilivyoko hapo langoni, papitapo watu wengi,

pua yako ni kama mnara wa Libanoni uelekeao Damasko.

5Kichwa chako hapa juu ni kama Karmeli,

nywele za kichwani pako ni nyekundu kama nguo za kifalme,

hata mfalme angependa kufungwa nayo hiyo misuko ya nywele.

6U mzuri peke yako kwa kupendeza sana,

mpenzi wangu, unazidisha mambo yafurahishayo.

7Hivyo, ulivyokua, unafanana na mtende,

nayo maziwa yako yanafanana na vichala vya mzabibu.

8Nilisema: Nitaupanda mtende huu, niyashike makuti yake,

maziwa yako yaniwie kama vichala vya mzabibu,

nao mnuko wa pumzi yako uniwie kama wa machungwa.

9Kinywa chako ni kama mvinyo njema

inayompendeza mpendwa wako, akiinywa,

nayo hupita polepole midomoni mwao walalao usingizi.”

10Mimi ni wake, mpendwa wangu, naye ananitunukia.[#Imbo. 2:16.]

11Njoo, mpendwa wangu, tutoke kwenda shambani, tulale vijijini![#Imbo. 2:10-13.]

12Na tuondoke mapema kwenda mizabibuni,

tutazame, kama mizabibu inachanua na kuyafunua maua.

tutazama nayo mikomamanga, kama imepata maua!

Hapo ndipo, nitakapokupa kukumbatiana na mimi.

13Mitunguja sasa inanuka, napo milangoni petu yapo matunda mazuri,

mapya na ya mwaka uliopita; ndiyo, niliyokuwekea, mpendwa wangu.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania