The chat will start when you send the first message.
1Tena Daudi na makamanda wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi kulingana na utumishi wao;[#1 Nya 12:28; 23:2; 6:33; 15:17; Kut 15:20; Hes 11:25; 1 Sam 10:5; 1 Nya 16:4; 23:5; Zab 150:3,5; 1 Kor 14:1; Ufu 15:2,4]
2wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme.
3Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu BWANA.
4Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;
5hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.[#1 Sam 9:9; 2 Sam 24:11; 1 Nya 21:9; 26:28; Amo 7:12; 1 Pet 4:11; Mwa 33:5; 1 Sam 1:17; 1 Nya 28:5; Zab 127:3; 128:3; Isa 3:18]
6Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.
7Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia BWANA, wote waliokuwa mastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.[#Zab 150:1; Efe 5:19; Kol 3:16; Yak 5:13]
8Wakapigiwa kura ya huduma zao, kwa pamoja, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.[#2 Nya 23:13]
9Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili;
10ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
11ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
12ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
13ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
14ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
15ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
16ya tisa Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili;
17ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
18ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
19ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
20ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
21ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
22ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
23ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
24ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
25ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
26ya kumi na tisa Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
27ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
28ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
29ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
30ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
31ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.[#Ufu 4:4; 5:8; 11:16]