1 Mambo ya Nyakati 27

1 Mambo ya Nyakati 27

Mgawanyo wa majeshi

1Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa koo za mababa, na makamanda wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lolote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu elfu ishirini na nne.

2Juu ya zamu ya kwanza ya mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu, mwana wa Zabdieli; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#2 Sam 23:8; 1 Nya 11:11]

3Yeye alikuwa wa wana wa Peresi, mkuu wa makamanda wote wa jeshi mwezi wa kwanza.[#Mwa 38:29]

4Na juu ya zamu ya mwezi wa pili alikuwa Dodai, Mwahohi, na zamu yake; na Miklothi alikuwa afisa mkuu; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#2 Sam 23:9]

5Kamanda wa tatu wa jeshi mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa Yehoyada, kuhani; alikuwa mkuu, na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#1 Fal 4:5]

6Huyo Benaya ndiye yule aliyekuwa shujaa wa wale thelathini, na juu ya wale thelathini; na katika zamu yake alikuwa Amizabadi mwanawe.[#2 Sam 23:20-23; 1 Nya 11:22]

7Kamanda wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, nduguye Yoabu, na Zebadia mwanawe baada yake; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#2 Sam 2:18,23; 23:24; 1 Nya 11:26]

8Kamanda wa tano wa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi, Mwizrahi; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.

9Kamanda wa sita wa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.[#2 Sam 23:26; 1 Nya 11:28]

10Kamanda wa saba wa mwezi wa saba alikuwa Heksi, Mpeloni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#1 Nya 11:27]

11Kamanda wa nane wa mwezi wa nane alikuwa Sibekai, Mhushathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#2 Sam 21:18; 1 Nya 11:29]

12Kamanda wa tisa wa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri, Mwanathothi, wa Wabenyamini; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#1 Nya 11:28]

13Kamanda wa kumi wa mwezi wa kumi alikuwa Maharai, Mnetofathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#2 Sam 23:28; 1 Nya 11:36]

14Kamanda wa kumi na moja wa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya, Mpirathoni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#2 Sam 23:30; 1 Nya 11:31]

15Kamanda wa kumi na mbili wa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heledi, Mnetofathi, wa Othnieli; na katika zamu yake walikuwa watu elfu ishirini na nne.[#1 Nya 11:30; Amu 3:9]

Viongozi wa makabila ya Israeli

16Wakuu wa makabila ya Israeli walikuwa hawa; wa Wareubeni, Eliezeri mwana wa Zikri; wa Wasimeoni, Shefatia mwana wa Maaka;

17wa Lawi, Hashabia mwana wa Kemueli; wa Haruni, Sadoki;[#1 Nya 26:30]

18wa Yuda, Elihu, mmojawapo wa nduguze Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli;[#1 Sam 16:6]

19wa Zabuloni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeremothi mwana wa Azrieli;

20wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia, wa nusu kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaya;

21wa nusu kabila la Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri;

22wa Dani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli.

23Lakini Daudi hakufanya hesabu ya waliokuwa na umri wa chini ya miaka ishirini; kwa kuwa BWANA alikuwa amesema, ya kwamba atawaongeza Israeli mfano wa nyota za mbinguni.[#Mwa 15:5; Kut 32:13; Kum 1:10; 10:22; Ebr 11:12]

24Yoabu, mwana wa Seruya, alianza kuwahesabu, lakini hakumaliza; na ghadhabu ikawapata Israeli kwa hayo; wala hesabu hiyo haikuingizwa katika kumbukumbu za mfalme Daudi.[#2 Sam 24:15; 1 Nya 21:7]

Maofisa wengine

25Na juu ya hazina za mfalme alikuwa Azmawethi mwana wa Adieli; na juu ya hazina za mashambani, za mijini, na vijijini, na ngomeni, alikuwa Yonathani mwana wa Uzia;

26na juu ya hao wenye kazi ya kulima shamba alikuwa Ezri mwana wa Kelubu;

27na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi;[#Wim 8:11]

28na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi;

29na juu ya mifugo iliyolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya mifugo iliyokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai;

30na juu ya ngamia alikuwa Obili, Mwishmaeli; na juu ya punda alikuwa Yedeya, Mmeronothi;

31na juu ya makundi ya kondoo alikuwa Yazizi, Mhagri. Hao wote walikuwa watumishi wa akiba alizokuwa nazo mfalme Daudi.

32Naye Yonathani, mjombawe Daudi, alikuwa mshauri, na mtu wa akili, na mwandishi; Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa pamoja na wana wa mfalme;[#2 Sam 21:21]

33na Ahithofeli alikuwa mshauri wake mfalme; na Hushai, Mwarki, alikuwa rafiki yake mfalme;

34na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya