The chat will start when you send the first message.
1Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli;[#1 Sam 25:43; 27:3; 2 Sam 3:2; Yos 15:56]
2wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi;
3wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe.[#2 Sam 3:5]
4Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akatawala miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.[#2 Sam 2:11; 1 Fal 2:11; 2 Sam 5:5]
5Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;[#1 Nya 14:4; 2 Sam 12:24]
6na Ibhari, na Elishua, na Elipeleti;
7na Noga, na Nefegi, na Yafia;
8na Elishama, na Eliada, na Elifeleti, watu tisa.[#2 Sam 5:14]
9Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wana wa masuria; na Tamari alikuwa dada yao.[#2 Sam 13:1; 14:27]
10Na wazawa wa Sulemani walikuwa: Rehoboamu mwanawe; mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati;[#1 Fal 11:43; 14:31; 15:6]
11na mwanawe huyo ni Yehoramu; na mwanawe huyo ni Ahazia; na mwanawe huyo ni Yoashi;
12na mwanawe huyo ni Amazia; na mwanawe huyo ni Uzia; na mwanawe huyo ni Yothamu;
13na mwanawe huyo ni Ahazi; na mwanawe huyo ni Hezekia; na mwanawe huyo ni Manase;
14na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia.
15Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
16Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia.[#Mt 1:11; 2 Fal 24:17]
17Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli,[#Mt 1:12]
18na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia.
19Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa dada yao;[#Ezr 3:2]
20na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.
21Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.[#3:21 Au, hivi, Na wana wa Hanania; Pelatia, na mwanawe huyo ni Yeshaya, na mwanawe huyo ni Refaya, na mwanawe huyo ni Arnani, na mwanawe huyo ni Obadia, na mwanawe huyo ni Shekania.]
22Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita.[#Ezr 8:2]
23Na wana wa Nearia; Elioenai, na Hezekia, na Azrikamu, watu watatu.
24Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.