1 Mambo ya Nyakati 7

1 Mambo ya Nyakati 7

Wazawa wa Isakari

1Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne.[#Mwa 30:17,18; 46:13; Hes 26:23]

2Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa koo za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita.[#2 Sam 24:1,2; 1 Nya 21:1-5; 27:1]

3Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu.[#1 Nya 5:24]

4Na pamoja nao, katika vizazi vyao, kulingana na koo za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu elfu thelathini na sita; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi.

5Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu elfu themanini na saba.

Wazawa wa Benyamini

6Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu.[#Mwa 46:21; Hes 26:38; 1 Nya 8:1]

7Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu elfu ishirini na mbili na thelathini na wanne.

8Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri.

9Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu elfu ishirini na mia mbili.

10Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari.

11Hao wote ndio wana wa Yediaeli, kulingana na wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, elfu kumi na saba na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.

12Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri.[#Hes 26:38,39]

Wazawa wa Naftali

13Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shalumu; wana wa Bilha.[#Mwa 46:24]

Wazawa wa Manase

14Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;[#Hes 27:1]

15naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao dada yao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.[#Hes 27:1-11]

16Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.

17Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.[#1 Sam 12:11]

18Na dada yake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.

19Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.

Wazawa wa Efraimu

20Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi;[#Mwa 41:52; 48:14-20; Hes 26:35,36; Kum 33:13,17; Zab 60:7; 108:8]

21na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuwapokonya ng'ombe wao.

22Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji.[#Mwa 37:34,35; Yos 7:6; 2 Sam 1:11; 3:31; Ayu 2:11; Zab 69:11; Yoe 2:13; Yn 11:19]

23Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu maafa yalikuwa yameipata nyumba yake.[#Mwa 35:18; 1 Sam 4:21; 1 Nya 4:9]

24Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.[#Yos 16:3; 1 Sam 13:18; 2 Nya 8:5]

25Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani;

26na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama;

27na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.[#Hes 13:8,16]

28Na hizi ndizo miliki yao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;

29na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli.[#Yos 17:7,11; 1 Fal 9:15; Amu 1:22-29]

Wazawa wa Asheri

30Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na dada yao, Sera.[#Mwa 46:17; 49:20; Hes 26:44,46; Kum 33:24]

31Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.

32Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na dada yao, Shua.

33Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti.

34Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu.

35Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali.

36Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra;

37na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera.

38Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara.

39Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia.

40Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa koo za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, viongozi wa wakuu. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu elfu ishirini na sita.[#Kum 2:14]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya