The chat will start when you send the first message.
1Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
2kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.[#Mdo 18:1; 1 Kor 6:11; Mdo 9:14]
3Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.[#Rum 1:7]
4Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu;
5kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote;
6kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu;
7hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;[#Lk 17:30; 2 The 1:7; Tit 2:13]
8ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.[#Flp 1:6; 1 The 3:13; 5:23]
9Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.[#1 The 5:24; 1 Yoh 1:3]
10Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu migawanyiko, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.[#Flp 2:2; 3:16]
11Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba uko ugomvi kwenu.
12Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.[#Mdo 18:24,27; 1 Kor 3:4; Yn 1:42]
13Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
14Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo;[#Mdo 18:8; 19:29; Rum 16:23]
15mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu.
16Tena niliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nilimbatiza mtu yeyote mwingine.[#1 Kor 16:15]
17Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.[#Yn 4:2; Mt 28:19]
18Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.[#2 Kor 4:3; Rum 1:16]
19Kwa kuwa imeandikwa,[#Isa 29:14]
Nitaiharibu hekima yao wenye hekima,
Na akili zao wenye akili nitazikataa.
20Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi mleta hoja wa nyakati hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?[#Ayu 12:17; Isa 19:12; 33:18; 44:25]
21Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.[#Mt 11:25; Lk 8:12]
22Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wagiriki wanatafuta hekima;[#Mt 12:38; Yn 4:48; Mdo 17:18,32]
23bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulubiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wagiriki ni upuzi;[#1 Kor 2:14; Rum 9:32]
24bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wagiriki, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.[#Kol 2:3]
25Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.[#2 Kor 13:4]
26Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;[#Mt 11:25; Yn 7:48; Yak 2:1-5]
27bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
28tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
29mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.[#Rum 3:27; Efe 2:9]
30Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;[#Yer 23:5,6; 2 Kor 5:21; Yn 17:19]
31kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.[#Yer 9:23,24]