The chat will start when you send the first message.
1Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;[#2 Yoh 1:1; 3 Yoh 1:1; Rum 8:17; Ufu 1:9]
2lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.[#Yn 10:12; 21:15-17; Flm 1:14; Tit 1:11; Mdo 20:28; 1 Tim 3:2-7]
3Wala si kama wajifanyao mabwana wa wale walio chini ya utunzaji wao, bali iweni mifano kwa lile kundi.[#2 Kor 1:24; Tit 2:7; Flp 3:17; 1 The 1:7]
4Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtalipokea taji la utukufu, lile lisilokauka.[#1 Pet 2:25; Ebr 13:20; 1 Kor 9:25; 2 Tim 4:8]
5Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.[#Mit 3:34; Efe 5:21; Mt 23:12; Yn 13:4,14; Yak 4:6]
6Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;[#Mt 23:12; Lk 14:11; 18:14; Ayu 22:29; Yak 4:10]
7huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.[#Zab 55:22; Mt 6:25; Flp 4:6]
8Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.[#1 The 5:6; Lk 18:3; Yak 4:7]
9Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu kote duniani.[#Efe 6:11-13]
10Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.[#1 Pet 1:6; 1 The 2:12]
11Uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
12Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nijuavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.[#Mdo 15:22,40; Ebr 13:22]
13Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.[#Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; Kol 4:10; Flm 1:24; 2 Tim 4:11]
14Salimianeni kwa busu la upendo.[#1 Kor 16:20]
Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina.