The chat will start when you send the first message.
1Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu,[#Efe 1:1]
2kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.[#Rum 1:7; Efe 1:2]
3Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea;[#1 Kor 13:13; Efe 1:16; 1 The 1:2,3]
4tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;[#Efe 1:15]
5kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;[#1 Pet 1:4; Efe 1:13,18]
6iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;[#1 Tim 3:16; Efe 1:13]
7kama mlivyofundishwa na Epafra, mwenzi wetu mpendwa, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu;[#Kol 4:12; Flm 1:23]
8naye alitueleza upendo wenu katika Roho.
9Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;[#Efe 1:8,9,15-17; Flp 1:9]
10mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;[#Efe 1:17; 2:10; 4:1; Flp 1:27]
11mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;[#1 Kor 1:5; Efe 1:18,19; 3:16]
12mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.[#Efe 1:11,18]
13Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa;[#Kol 2:15; Lk 22:53; Efe 2:2; 6:12; 1:6]
14ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.[#Efe 1:7]
15Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.[#Ebr 1:3; 2 Kor 4:4; 1 Tim 6:16; Yn 1:18]
16Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au milki, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.[#Yn 1:3,10; Efe 1:10,21]
17Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.[#Mit 8:25-27; Efe 1:22]
18Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.[#Efe 1:22-23; 4:15; 5:23; Mdo 4:2; 26:23; Ufu 1:5]
19Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;[#Efe 1:23; Kol 2:9; Yn 1:16]
20na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.[#Efe 1:7,10; 2:13,16; 1 Yoh 2:2]
21Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmetengwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;[#Efe 2:1,12; 4:18; Rum 5:10]
22katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama;[#Efe 2:11,14,16; 5:27]
23mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa kwa viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nilikuwa mhudumu wake.[#Mk 16:15; 1 Tim 3:16; Efe 3:17; Ebr 3:14]
24Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake;[#Efe 3:1,13]
25ambalo nimefanywa mhudumu wake, kulingana na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu;[#Efe 3:2,7,8]
26siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake;[#Rum 16:25,26; Efe 3:3,5,9,10]
27ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu[#1 Tim 1:1; Rum 16:25; Efe 3:9; 1:18]
28ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.[#Efe 4:13]
29Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.[#Flp 4:13; Efe 3:7,20]