The chat will start when you send the first message.
1Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa,[#Sef 2:12]
Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi;
2Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari,
Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji.
Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini;
Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa;
Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu,
Ambao mito inakata nchi yao.
3Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni.
4Maana BWANA ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika joto la mavuno.
5Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.
6Wote pamoja wataachiwa ndege wakali wa milimani, na wanyama wa nchi; ndege wakali watakaa juu yao wakati wa jua, na wanyama wote wa nchi watakaa juu yao wakati wa baridi.
7Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hidaya na watu warefu, laini;[#Zab 68:31; Sef 3:10; Mal 1:11]
Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa;
Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu,
Ambao mito inagawanya nchi yao;
Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.