The chat will start when you send the first message.
1Basi, hawa ndio makuhani na Walawi waliopanda na Zerubabeli, mwana wa Shealueli, na Yoshua; Seraya, Yeremia, Ezra;[#Ezr 2:1; Neh 10:2-8]
2Amaria, Maluki, Hatushi;
3Shekania, Harimu, Meremothi;
4Ido, Ginethoni, Abia;[#Lk 1:5]
5Miyamini, Maazia, Bilgai;
6Shemaya, Yoyaribu, Yedaya;
7Salu, Amoki, Hilkia, Yedaya. Hawa walikuwa wakuu wa makuhani na ndugu zao siku za Yoshua.[#Hag 1:1; Zek 3:1]
8Tena Walawi; Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa juu ya shukrani, yeye na ndugu zake.[#1 Nya 16:8,41; Neh 11:17]
9Tena Bakbukia na Uno, washiriki wenzao walisimama mkabala wao.
10Naye Yoshua akamzaa Yoyakimu, Yoyakimu akamzaa Eliashibu, Eliashibu akamzaa Yoyada,
11Yoyada akamzaa Yohana, Yohana akamzaa Yadua.
12Na siku za Yoyakimu wakawako makuhani, wakuu wa mbari za mababa; wa Seraya, Meraya; wa Yeremia, Hanania;
13wa Ezra, Meshulamu; wa Amaria, Yehohanani;
14wa Maluki, Yonathani; wa Shekania, Yusufu;
15wa Harimu, Adna; wa Meremothi, Helkai;
16wa Ido, Zekaria; wa Ginethoni, Meshulamu;
17wa Abia, Zikri; wa Miyamini; wa Maazia, Piltai;
18wa Bilgai, Shamua; wa Shemaya, Yehonathani;
19wa Yoyaribu, Matenai; wa Yedaya, Uzi;
20wa Salu, Kalai; wa Amoki, Eberi;
21wa Hilkia, Hashabia; wa Yedaya, Nethaneli.
22Walawi siku za Eliashibu, na Yoyada, na Yohana, na Yadua, wameorodheshwa wakuu wa mbari za mababa; tena na makuhani; hata siku za kumiliki kwake Dario, Mwajemi.
23Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu hadi siku za Yohana mwana wa Eliashibu.[#1 Nya 9:14]
24Nao wakuu wa Walawi; Hashabia, Sherebia, Yeshua, Binui, Kadmieli, na ndugu zao kuwaelekea, ili kusifu na kushukuru, kama amri ya Daudi, mtu wa Mungu, zamu kwa zamu.[#1 Nya 23:1; 25:1; Ezr 3:11]
25Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni, na Akubu, walikuwa mabawabu, wa kulinda nyumba za hazina katika malango.
26Hao walikuwapo siku za Yoyakimu, mwana ya Yoshua, mwana wa Yosadaki, na siku za Nehemia, mtawala, na Ezra, kuhani na mwandishi.[#Neh 8:9; Ezr 7:6,11]
27Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, ili waweze kusherehekea kuweka wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi.[#Kum 20:5; 1 Nya 25:6; 2 Nya 5:13; Zab 81:1-3; Ufu 5:8]
28Waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya Yerusalemu, na kutoka vijiji vya Wanetofathi;
29tena kutoka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi; kwa maana waimbaji hao walikuwa wamejijengea vijiji katika viunga vya Yerusalemu.
30Makuhani na Walawi wakajitakasa, nao wakawatakasa watu, na malango, na ukuta.[#Kut 19:10]
31Ndipo nikawapandisha viongozi wa Yuda juu ya ukuta, nikawatenga makundi mawili makubwa ya hao walioandamana na kushukuru, liende upande wa kulia ukutani kuliendea lango la jaa;[#Neh 2:13]
32na baada yao wakaenda Hoshaya, na nusu ya wakuu wa Yuda,
33na Azaria, na Ezra, na Meshulamu,
34na Yuda, na Benyamini, na Shemaya, na Yeremia,
35na baadhi ya makuhani wenye baragumu; Zekaria, mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu;[#Hes 10:2; Yos 6:4; 2 Nya 5:12]
36na ndugu zake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda, na Hanani, wenye vinanda vya Daudi mtu wa Mungu; Ezra, mwandishi, akawatangulia;[#1 Nya 23:5; 2 Nya 8:14; Amo 6:5]
37na kwa lango la chemchemi, wakienda moja kwa moja mbele yao, wakapanda madaraja ya mji wa Daudi, uinukapo ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, mpaka lango la maji upande wa mashariki.[#Neh 2:14; 2 Sam 5:7-9; Neh 3:15,26]
38Na kundi la pili wao wenye kushukuru wakaenda kuwalaki, na mimi nikafuata nyuma yao, pamoja na nusu ya watu, ukutani juu ya mnara wa tanuri, mpaka ule ukuta mpana;[#Neh 3:8,11]
39na juu ya lango la Efraimu, na kupita lango la kale, na lango la samaki, na mnara wa Hananeli, na mnara wa Hamea, mpaka lango la kondoo; nao wakasimama hapo langoni pa gereza.[#2 Fal 14:13; Neh 3:6; Yer 32:2]
40Ndivyo walivyosimama makundi mawili yao walioshukuru nyumbani mwa Mungu, na mimi, na nusu ya viongozi pamoja nami;[#Zab 42:4]
41na makuhani, Eliakimu, Maaseya, Miyamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania, wenye baragumu;
42na Maaseya, na Shemaya, na Eleazari, na Uzi, na Yehohanani, na Malkiya, na Elamu, na Ezeri. Waimbaji wakaimba kwa sauti kuu, akiwa Yezrahia msimamizi wao.
43Wakatoa dhabihu nyingi siku ile, wakafurahi; kwa kuwa Mungu amewafurahisha furaha kuu; na wanawake pia na watoto wakafurahi; hata ikasikika mbali sana furaha hiyo ya Yerusalemu.[#Zab 9:2; 92:4]
44Na siku hiyo watu wakaagizwa juu ya vyumba vya hazina, kwa sadaka za kuinuliwa, na kwa malimbuko, na kwa zaka, ili kuzikusanya, kwa kadiri ya mashamba ya miji, sehemu zilizoamriwa katika torati za makuhani, na Walawi; kwa maana Yuda waliwafurahia makuhani na Walawi waliotumika.[#2 Nya 13:11,12; Neh 13:5]
45Wakauangalia ulinzi wa Mungu wao, na ulinzi wa kutakasika, na hao waimbaji na mabawabu vile vile, sawasawa na amri ya Daudi, na ya Sulemani mwanawe.[#1 Nya 25:1]
46Kwa kuwa siku za Daudi zamani, Asafu alikuwa mkuu wa waimbaji, na juu ya nyimbo za sifa na shukrani kwa Mungu.
47Na Israeli wote, siku za Zerubabeli, na siku za Nehemia, walitoa sehemu za waimbaji na mabawabu, kama ilivyohusika kila siku; nao wakawatakasia Walawi; na Walawi wakawatakasia wana wa Haruni.