The chat will start when you send the first message.
1Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
3Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
4Kwa manyoya yake atakufunika,[#Zab 61:4]
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5Hutaogopa hatari za usiku,[#Ayu 5:19; Mit 3:23; Isa 43:2]
Wala mshale urukao mchana,
6Wala mapigo yajayo usiku,
Wala maafa yatokeayo adhuhuri,
7Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako.
Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia!
Wewe hutakaribiwa na maafa.
8Ila kwa macho yako utatazama,[#Mal 1:5]
Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;
Umemfanya Aliye Juu kuwa makao yako.
10Mabaya hayatakupata wewe,[#Mit 1:33; 2 The 3:3; 2 Pet 2:9]
Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11Kwa kuwa atakuagizia malaika wake[#Mt 4:6; Lk 4:10]
Wakulinde katika njia zako zote.
12Mikononi mwao watakuchukua,[#Ayu 5:23; Zab 37:24; Mt 4:6; Lk 4:11]
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13Utawakanyaga simba na nyoka,[#Lk 10:19]
Mwanasimba na joka utawakanyaga kwa miguu.
14Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,
Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15Ataniita nami nitamwitikia;[#Ayu 22:27; Zab 18:3; Yer 33:3; Zek 13:9; Ebr 5:7; Zab 43:2; 1 Sam 2:30]
Nitakuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza;
16Kwa siku nyingi nitamshibisha,
Nami nitamwonesha wokovu wangu.