Zaburi 98

Zaburi 98

Sifa kwa mwamuzi wa Dunia

1Mwimbieni BWANA wimbo mpya,[#Isa 59:16]

Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.

Mkono wa kulia,

Na mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.

2BWANA ameufunua wokovu wake,[#Isa 52:10; Lk 2:30; Isa 62:2; Rum 3:25; Law 26:45; Kum 4:31; Mik 7:20; Lk 1:54; Isa 49:6; Lk 3:6; Mdo 13:47]

Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.

3Amezikumbuka rehema zake,

Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.

Miisho yote ya dunia imeuona

Wokovu wa Mungu wetu.

4Mshangilieni BWANA, nchi yote,

Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni sifa.

5Mwimbieni BWANA sifa kwa kinubi,

Kwa kinubi na sauti tamu.

6Kwa panda na sauti ya baragumu.[#Hes 10:10; 1 Nya 15:28; 2 Nya 29:27]

Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.

7Bahari na ivume na vyote viijazavyo,

Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.

8Mito na ipige makofi,

Milima na iimbe pamoja kwa furaha.

9Mbele za BWANA;

Kwa maana anakuja kuihukumu nchi.

Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu,

Na mataifa kwa adili.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya