The chat will start when you send the first message.
1Adamu, na Sethi, na Enoshi;[#Mwa 4:25; 5:3,9]
2na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi;
3na Henoko, na Methusela, na Lameki;[#Yud 1:14]
4na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.
5Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.[#Mwa 10:2]
6Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
7Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.
8Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.[#Mwa 16:0]
9Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani.
10Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.[#Mwa 10:8,13]
11Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
12na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.[#Mwa 10:14; Kum 2:23; Yer 47:4; Amo 9:7]
13Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;
14na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;
15na Mhivi, na Mwarki, na Msini;
16na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.[#Mwa 9:23,26; 10:22; 11:10]
18Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi.
19Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani.
20Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera;
21na Hadoramu, na Uzali, na Dikla;
22na Obali, na Abimaeli, na Sheba;
23na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24Shemu, na Arfaksadi, na Sala;[#Mwa 11:10; Lk 3:36]
25na Eberi, na Pelegi, na Reu;[#Mwa 11:15; Hes 24:24; Lk 3:35]
26na Serugi, na Nahori, na Tera;
27na Abramu, naye ndiye Abrahamu.[#Mwa 17:5; 2 Nya 20:7; Neh 9:7; Isa 41:8; 51:2; Rum 4:16; Yak 2:23]
28Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli.[#Mwa 21:2,3; 16:11,15]
29Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu;[#Mwa 25:13-16]
30na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema;[#Mwa 25:15]
31na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.[#Mwa 25:1,2]
33Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.
34Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.[#Mwa 21:2,3; 25:25]
35Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora.[#Mwa 36:9,10; Kum 2:22; Mal 1:2,3; Rum 9:13; Ebr 12:16]
36Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.[#Mwa 36:11]
37Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza.
38Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani.[#Mwa 36:20]
39Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani.[#Mwa 36:22]
40Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana.[#Mwa 36:23]
41Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.[#Mwa 36:25,26]
42Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.[#Mwa 36:27]
43Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.[#Mwa 36:31; 49:10]
44Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake.
45Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake.
46Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi.[#1 Fal 11:14]
47Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake.
48Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake.[#Mwa 36:37]
49Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake.
50Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.[#Mwa 36:39]
51Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi;[#Mwa 36:40; Kut 15:15]
52na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni;
53na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari;
54na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.