1 Mambo ya Nyakati 9

1 Mambo ya Nyakati 9

1Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.[#Ezr 2:59; Neh 7:5; Law 26:33; 2 Nya 33:11; 36:5]

2Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika miliki yao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.[#Ezr 2:70; Neh 7:73; Yos 9:27; Ezr 2:43; 8:20]

Wakazi wa Yerusalemu baada ya uhamisho

3Na huko Yerusalemu walikuwa wakikaa baadhi ya wana wa Yuda, na wana wa Benyamini, na wana wa Efraimu na Manase;[#Neh 11:1]

4Uthai, mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imli, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.[#Mwa 46:12; Hes 26:20]

5Na wa Washiloni; Asaya, mzaliwa wa kwanza, na wanawe.

6Na wa wana wa Zera; Yeueli, na ndugu zao; watu mia sita na tisini.

7Na wa wana wa Benyamini; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;

8na Ibneya, mwana wa Yerohamu; na Ela, mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu, mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya;

9na ndugu zao, kulingana na vizazi vyao; watu mia tisa na hamsini na sita. Watu hao wote ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, kwa kadiri ya mbari za baba zao.

Familia za ukuhani

10Na katika makuhani; Yedaya, na Yehoyaribu, na Yakini;[#Neh 11:10; 12:19]

11na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;

12na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; na Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yazera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri;

13wakuu wa koo za baba zao; pamoja na ndugu zao; watu elfu moja na mia saba na sitini; watu wenye ujuzi waliofaa sana kwa kazi ya huduma ya nyumba ya Mungu.

Jamii za Walawi

14Na katika Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari;[#1 Nya 6:19; Neh 11:15-19]

15na Bakbakari, na Hereshi, na Galali, na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu;

16na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.[#1 Nya 2:54; Neh 7:26; 12:28]

17Na katika mabawabu; Shalumu, na Akubu, na Talmoni, na Ahimani, na ndugu zao; naye Shalumu alikuwa mkuu wao;[#1 Nya 23:5; 26:1; Zab 84:10]

18ambao tangu hapo walikuwa wakilinda penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa walinzi wa kambi ya wana wa Lawi.[#2 Fal 11:19; Eze 44:23]

19Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa ukoo wa babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ulinzi wa malango ya maskani; na kama vile baba zao walivyokuwa wamesimamia kambi ya BWANA, wakiyalinda maingilio;[#Hes 26:9,11; 1 Nya 6:33,38]

20naye Finehasi, mwana wa Eleazari, alikuwa mkuu wao hapo zamani, naye BWANA alikuwa pamoja naye.[#Kut 6:25; Hes 3:32; 25:11; 31:6; Yos 22:30,31; Zab 106:30]

21Zekaria, mwana wa Meshelemia, alikuwa bawabu mlangoni pa ile hema ya kukutania.

22Hao wote waliochaguliwa kuwa walinzi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyotegemewa kwayo.[#1 Nya 26:1,2; 1 Sam 9:9]

23Basi watu hao na wana wao walikuwa na kazi ya ulinzi wa malango ya nyumba ya BWANA, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.

24Hao walinzi walikuwapo pande zote nne, kuelekea mashariki, na magharibi, na kaskazini, na kusini.[#1 Nya 26:13-19]

25Na ndugu zao, katika vijiji vyao, wakawajibika kuingia kila siku ya saba, zamu kwa zamu, ili kuwa pamoja nao;[#2 Fal 11:5; 2 Nya 23:8]

26kwa maana wale walinzi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, waliwajibika kuvilinda vyumba na hazina ya nyumba ya Mungu.

27Nao walilala kandokando nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa ulinzi wake ulikuwa juu yao, nayo ilikuwa kazi yao kuyafungua malango kila siku asubuhi.

28Na baadhi yao walivilinda vyombo vya huduma; kwani huingizwa kwa hesabu, na kutolewa kwa hesabu vile vile.

29Na baadhi yao waliwajibika kuviangalia vyombo vya nyumbani, na vyombo vyote vya Patakatifu; pamoja na unga safi, na divai, na mafuta, na ubani, na manukato.

30Na baadhi ya wana wa makuhani waliyatayarisha manukato.[#Kut 30:23; 37:29; Wim 1:3,13; Yer 6:20; Eze 27:19,22; Mk 14:3]

31Naye Matithia, Mlawi mmojawapo, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, Mkora, aliwajibika kusimamia uokaji wa mikate myembamba.[#Law 6:21]

32Na baadhi ya ndugu zao, wa wana wa Wakohathi, waliwajibika kusimamia mikate ile ya wonyesho, ili kuiandaa kila sabato.[#Kut 40:23; Ebr 9:2,24; Yn 6:32,33]

33Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walifanya kazi yao mchana na usiku.[#1 Nya 6:31; 13:8; 15:16]

34Hao walikuwa wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, katika vizazi vyao vyote, watu wakuu; nao walikuwa wakikaa huko Yerusalemu.

Jamaa wa mfalme Sauli

35Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, na jina la mkewe aliitwa Maaka;[#1 Nya 8:29]

36na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni; na Suri, na Kishi, na Baali, na Meri, na Nadabu;

37na Gedori, na Ahio, na Zekaria, na Miklothi.

38Na Miklothi akamzaa Shimea. Hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.

39Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.[#1 Nya 8:33]

40Na mwana wa Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.

41Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea.[#2 Sam 9:12; 1 Nya 8:35; #9:41 tazama 1 Nya 8:35.]

42Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;

43na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli;

44naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya