The chat will start when you send the first message.
1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.[#Mt 17:20; 7:22; 21:21; Mk 11:23]
3Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.[#Mt 6:2]
4Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;[#Zek 8:17; Flp 2:4]
6haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;[#Rum 12:9]
7huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.[#Mit 10:12; 1 Kor 9:12; Rum 15:1]
8Upendo haupungui neno wakati wowote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.[#1 Pet 4:8]
9Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;
10lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.
11Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
12Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.[#2 Kor 5:7; Yak 1:23]
13Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.[#1 The 1:3; 1 Yoh 4:16]