The chat will start when you send the first message.
1Samweli akamwambia Sauli, BWANA alinituma nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya BWANA.[#1 Sam 10:1; 9:16]
2BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu yale ambayo Waamaleki waliwatenda Waisraeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri.[#Kut 17:8-14; Kum 25:17-19]
3Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.[#Law 27:28; Yos 6:17; Kut 20:5; Isa 14:21; Mwa 3:17; Yos 7:24]
4Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari wa miguu elfu mia mbili na watu elfu kumi wa Yuda.[#Yos 15:24]
5Sauli akaufikia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni.
6Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Nendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki.[#Hes 24:21; Amu 1:16; 4:11; Mwa 18:25; 19:12; Mdo 2:40; Ufu 18:4; Kut 18:10; Hes 10:29]
7Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila hadi Shuri, mashariki mwa Misri.[#1 Sam 14:48; Mwa 2:11; 25:18; 16:7; 1 Sam 27:8]
8Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki akiwa hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga.[#1 Fal 20:34; Est 3:1; 1 Sam 30:1]
9Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.[#Mit 15:27; 1 Tim 6:10]
10Ndipo neno la BWANA likamjia Samweli, kusema,
11Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.[#Mwa 6:6; 2 Sam 24:16; Yos 22:16; 1 Fal 9:6; Zab 36:3; Sef 1:6; Mt 24:13; 1 Sam 16:1; Lk 19:41,44; Rum 9:1-3]
12Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia mnara wa ukumbusho wake, akageuka, akapita, akateremkia Gilgali.[#Yos 15:55]
13Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA.[#Mwa 14:19; Amu 17:2; Rut 3:2; Lk 18:11]
14Samweli akasema, Maana yake nini basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia?
15Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.[#Mwa 3:12; Mit 28:13]
16Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia BWANA usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema.
17Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.
18Kisha BWANA akakutuma safarini, akasema, Nenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hadi watakapoangamia.
19Mbona basi hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA?
20Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa.
21Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.
22Naye Samweli akasema,[#Zab 50:8,9; Mit 21:3; Isa 1:11; Yer 7:22; Amo 5:21,24; Mik 6:6; Mt 9:13; 12:7; Ebr 10:6; Kut 19:5; Mhu 5:1; Yer 7:23; Hos 6:6; Mt 5:24; 9:13; Mk 12:33]
Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.
23Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,[#Kum 18:10]
Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago;
Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA,
Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
24Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeivunja amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu niliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.[#2 Sam 12:13; Kut 9:27; Mt 27:4; Kut 23:2; Ayu 31:34; Mit 29:25; Isa 51:12; Lk 23:20-25; Ufu 21:8]
25Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA.
26Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.[#1 Sam 2:30]
27Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka.[#1 Sam 28:17; 1 Fal 11:30-31]
28Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.
29Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.[#Hes 23:19; Eze 24:14; 2 Tim 2:13; Tit 1:2]
30Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako.[#1 Sam 2:30; Zab 49:20; Mit 4:8; 26:1; Yn 5:44; 12:43; Rum 2:28,29]
31Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA.
32Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa ulegevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka.[#15:32 maana katika Kiebrania si dhahiri.]
33Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali.[#Mwa 9:6; Kut 17:11; Amu 1:7; Mt 7:2; Yak 2:13; Ufu 16:6; 18:6; 1 Fal 18:40]
34Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli.[#1 Sam 11:4]
35Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye BWANA akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.