The chat will start when you send the first message.
1Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.
2Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote BWANA aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote;
3yale majaribu makuu yaliyoyaona macho yako; hizo ishara, na ile miujiza mikuu;[#Kum 4:34; 7:19]
4lakini BWANA hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi.[#Zab 13:3; 19:8; Isa 6:9; 63:17; Eze 12:2; Mt 13:14; Yn 8:43; Mdo 28:26; Rum 11:8; Efe 1:18; 4:17-19; 2 The 2:11]
5Nami miaka arubaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.[#Kum 1:3; 8:2]
6Hamkula mkate, wala hamkunywa divai, wala kileo; ili mpate kujua kwamba Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.[#Kut 16:12; Neh 9:15; Zab 78:24]
7Nanyi mlipokuja mahali hapa, walitutokea kupigana juu yetu Sihoni mfalme wa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, tukawapiga;[#Hes 21:21-35; Kum 2:32; 3:1]
8tukaitwaa nchi yao, nayo tukawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila la Manase, iwe urithi.[#Hes 32:33]
9Shikeni basi maneno ya agano hili myafanye, ili mfanikiwe katika yote mfanyayo.[#Yos 1:7; 1 Fal 2:3; Zab 25:10; 103:17,18; Isa 56:1,2,4,7; Yer 1:5]
10Leo mmesimama nyote mbele za BWANA, Mungu wenu; wakuu wenu, na makabila yenu, na wazee wenu, na maofisa wenu, wanaume wote wa Israeli,
11vijana vyenu, na wake wenu, na mgeni wako aliye kati ya kituo chako, tokea mchanjaji wa kuni zako hata mtekaji wa maji yako;[#Yos 9:21]
12ili uingie katika agano la BWANA, Mungu wako, na kiapo chake, afanyacho nawe BWANA, Mungu wako, hivi leo;
13apate kukuweka leo uwe taifa kwake naye apate kuwa Mungu kwako, kama alivyokuambia, na kama alivyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.[#Mwa 17:6,7]
14Wala sifanyi na ninyi peke yenu agano hili na kiapo hiki;[#Yer 31:31; Ebr 8:7,8]
15ila na yeye aliyesimama hapa nasi hivi leo mbele ya BWANA, Mungu wetu, na yeye naye asiyekuwapo pamoja nasi leo;[#Mdo 2:39; 1 Kor 7:14]
16(kwani mwajua mlivyoketi nchi ya Misri, na tulivyo kuja katikati ya mataifa hayo mliyopita katikati yao;
17nanyi mliona machukizo yao, na sanamu zao, miti na mawe, fedha na dhahabu, zilizokuwako kwao;)
18asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache BWANA, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga;[#Ebr 12:15]
19ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu;[#Zab 14:1; Hes 15:39; Omb 3:39; Yer 7:24; Ayu 15:16; 34:7; Isa 30:1; 56:12; Efe 4:19]
20BWANA hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya BWANA na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA atalifuta jina lake chini ya mbingu.[#Eze 14:7; 23:25; Zab 74:1; 79:5]
21BWANA atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika kitabu hiki cha torati.[#Mt 24:51]
22Na kizazi cha baadaye, wanenu watakaoinuka baada yenu, na mgeni atakayekuja kutoka nchi ya mbali, watasema, watakapoyaona mapigo ya nchi ile, na magonjwa aliyoitia BWANA;
23ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake;[#Mwa 19:24-25; Amu 9:45; Zab 107:34; Yer 17:6; Eze 47:11; Sef 2:9; Lk 14:34,35]
24mataifa yote watasema, Mbona BWANA ameifanyia hivi nchi hii? Ni nini maana yake joto la hasira hizi kubwa?[#1 Fal 9:8; Yer 22:8]
25Ndipo watakaposema watu, Ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, Mungu wa baba zao, alilofanya nao hapo alipowatoa katika nchi ya Misri;
26wakaenda wakatumikia miungu mingine, wakaiabudu miungu wasiyoijua, asiyowapa yeye;
27ndipo ikawashwa hasira ya BWANA juu ya nchi hii, kwa kuleta juu yake laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki;[#Zab 11:6; Dan 9:11]
28BWANA akawang'oa katika nchi yao kwa hasira, na ghadhabu, na makamio makuu, akawatupa waende nchi nyingine, kama hivi leo.[#2 Nya 7:20; Ayu 11:6,7; Zab 52:5; Mit 2:22; 3:22]
29Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.[#Ayu 11:6,7; Mit 3:32; Yer 23:18; Amo 3:7; Mdo 1:7; Zab 19:7; Lk 16:29; Yn 5:39; Mdo 17:11; 2 Tim 3:16]