The chat will start when you send the first message.
1Hivyo mwigeni Mungu, kama watoto wanaopendwa;[#Mt 5:48; Kol 3:12]
2mkaende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.[#Kut 29:18; Zab 40:6; Gal 2:20; Ebr 10:10; Kol 3:13; Eze 20:41]
3Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;[#Efe 4:19; Kol 3:5]
4wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali kuwepo kushukuru.[#Efe 4:29; Kol 3:8]
5Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, (ndiye mwabudu sanamu), aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.[#1 Kor 6:9,10; Kol 3:5; Mdo 8:21]
6Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.[#Rum 1:18; Kol 2:4,8]
7Basi msishirikiane nao.
8Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; nendeni kama watoto wa nuru,[#Efe 2:11,13; Lk 16:8; 1 Pet 2:9; Yn 12:36]
9kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;
10mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.[#Rum 12:2]
11Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;[#Yn 16:8]
12kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.[#Rum 1:24]
13Lakini chochote kinachoangazwa na nuru hudhihirishwa, maana chochote kile kilichoadhihirika ni nuru.[#Yn 3:20,21]
14Hivyo husema,[#Isa 26:19; 60:1; Rum 13:11; 6:13]
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke katika wafu,
Na Kristo atakuangaza.
15Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;[#Mt 10:16; Kol 4:5]
16mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu.[#Kol 4:5]
17Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.[#Rum 12:2]
18Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;[#Mit 23:31; Lk 21:34]
19mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;[#Kol 3:16-17; Zab 33:2,3]
20na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.[#Kol 3:17]
21Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.[#1 Pet 5:5]
22Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.[#Kol 3:18; 1 Pet 3:1; Mwa 3:16]
23Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.[#1 Kor 11:3; Kol 1:18]
24Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake;[#Kol 3:19; 1 Pet 3:7]
26ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;[#Tit 3:5]
27apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na dosari wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.[#Zab 45:13; 2 Kor 11:2]
28Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa.
30Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.[#Efe 1:23; 1 Kor 6:15; Mwa 2:23]
31Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.[#Mwa 2:24]
32Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na kanisa.[#Ufu 19:7]
33Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.