The chat will start when you send the first message.
1BWANA akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.[#Kut 11:1; 12:31]
2Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni BWANA;[#Mwa 17:1; 28:3; 35:11; Kut 3:13-15]
3nami nilimtokea Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.[#Zab 68:4; Yn 8:58; Ufu 1:4; #6:3 Katika Kiebrania ni ‘EL-SHADDAI’ ‘Mungu Mwenyezi’ au ‘Mungu mwenye nguvu’.]
4Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya waliyokaa kama wageni.[#Mwa 15:18; 17:4,7,8]
5Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.[#Kut 2:24]
6Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni BWANA nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya ukandamizaji wa Wamisri, nami nitawaokoa kutoka utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;[#Kut 3:17; 7:4; 15:13; Kum 26:8; 7:8; Zab 81:6; 136:11; 1 Nya 17:21; Neh 1:10]
7nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwakomboaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.[#Kum 7:6; 29:13; 2 Sam 7:24; Mwa 17:7,8; Ufu 21:7; Zab 81:6]
8Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo niliinua mkono wangu, niwape Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.[#Mwa 15:18; 26:3]
9Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
10BWANA akasema na Musa, akamwambia,
11Ingia ndani, ukaseme na Farao, mfalme wa Misri, ili awape ruhusa wana wa Israeli watoke nchi yake.
12Musa akanena mbele za BWANA, akasema, Tazama, hao wana wa Israeli hawakunisikiza mimi; basi huyo Farao atanisikizaje, mimi niliye na midomo isiyo tohara?[#Yer 1:6; #6:12 ‘Mimi niliye na kigugumizi au asiye na ufasaha wa kuhutubia’.]
13BWANA akanena na Musa na Haruni, akawaagiza wawaendee wana wa Israeli, na Farao, mfalme wa Misri, ili awatoe hao wana wa Israeli katika nchi ya Misri.
14Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni.[#Mwa 49:9; 1 Nya 5:3]
15Na wana wa Simeoni; ni Yemueli, na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli mwana wa mwanamke wa Kikanaani; hao ni jamaa za Simeoni.[#Mwa 46:10; 1 Nya 4:24]
16Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na vizazi vyao; Gershoni, na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.[#Hes 3:17-20; 26:57-58; 1 Nya 6:16-19; Mwa 46:11; 1 Nya 6:1; #6:16 Pengine huitwa ‘Gershomu’ Tafsiri yake ni ‘mkimbizi’ tazama Kut 2:22.]
17Wana wa Gershoni; ni Libni, na Shimei, kulingana na jamaa zao.
18Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.[#Hes 26:57; 1 Nya 6:18]
19Na wana wa Merari; ni Mali, na Mushi. Hizi ni jamaa za hao Walawi kulingana na vizazi vyao.
20Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.[#Kut 2:1,2; Hes 26:59]
21Na wana wa Ishari; ni Kora, na Nefegi, na Zikri.[#Hes 16:1; 1 Nya 6:37,38]
22Na wana wa Uzieli; ni Mishaeli, na Elisafani, na Sithri.[#Law 10:4; Hes 3:30]
23Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.[#Rut 4:19,20; 1 Nya 2:10; Mt 1:4; Law 10:1; Hes 3:2]
24Na wana wa Kora; ni Asiri, na Elkana, na Abiasafu; hizo ni jamaa za hao Wakora.[#Hes 26:11]
25Na Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja miongoni mwa binti za Putieli; naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba wa Walawi kulingana na jamaa zao.[#Hes 25:7,11,12; Yos 24:33]
26Hawa ni Haruni yeye yule, na Musa yeye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao.[#Kut 7:4; 12:17; Hes 33:1]
27Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa yeye yule, na Haruni yeye yule.[#Kut 32:7; 33:1; Zab 77:20]
28Ilikuwa siku hiyo BWANA aliponena na Musa katika nchi ya Misri,
29BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA; mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo.[#Kut 7:2]
30Musa akanena mbele ya BWANA, Mimi ni mtu mwenye midomo isiyo tohara, Farao atanisikizaje?[#Kut 4:10; Yer 1:6]