Ezekieli 35

Ezekieli 35

Hukumu kwa mlima Seiri

1Tena neno la BWANA likanijia, kusema,[#Isa 34:5-17; 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; Amo 1:11-12; Oba 1-14; Mal 1:2-5]

2Mwanadamu, kaza uso wako juu ya mlima Seiri, ukatabiri juu yake,[#Amo 1:11; Oba 1:10]

3uuambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima Seiri, nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, nami nitakufanya kuwa ukiwa na ajabu.

4Miji yako nitaiharibu, nawe utakuwa ukiwa; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

5Kwa kuwa umekuwa na uadui usiokoma, nawe umewatoa wana wa Israeli wapigwe kwa nguvu za upanga, wakati wa msiba wao, wakati wa mwisho wa uovu.[#Zab 137:7]

6Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitakuweka tayari kwa damu, na damu itakufuatia; ikiwa hukuchukia damu, basi damu itakufuatia.[#Zab 109:17]

7Hivyo ndivyo nitakavyoufanya mlima Seiri kuwa ajabu na ukiwa; nami nitakatilia mbali nao mtu apitaye, na mtu arejeaye.

8Nami nitaijaza milima yake watu wake waliouawa; katika milima yako, na katika mabonde yako, na mito yako yote, wataanguka wao watakaouawa kwa upanga.

9Nitakufanya kuwa ukiwa wa daima, na miji yako haitakaliwa na watu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.[#Yer 49:17; Mal 1:3,4]

10Kwa sababu umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa BWANA alikuwako huko.[#Zab 83:4]

11Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitatenda kwa kadiri ya hasira yako, na kwa kadiri ya wivu wako, ulioudhihirisha kwa kuwachukia; nami nitajidhihirisha kwao, nitakapokuhukumu wewe.[#Mt 7:2; Isa 26:9]

12Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeyasikia matusi yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.[#Zab 9:16]

13Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa vinywa vyenu, na kuyaongeza maneno juu yangu; nimesikia mimi.

14Bwana MUNGU asema hivi; Dunia yote itakapofurahi, nitakufanya kuwa ukiwa.[#Isa 14:7,8]

15Kama vile ulivyofurahi juu ya urithi wa nyumba ya Israeli, kwa sababu ilikuwa ukiwa, ndivyo nitakavyokutenda wewe; utakuwa ukiwa, Ee mlima Seiri, na Edomu yote, naam, yote pia; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.[#Mit 17:5; Oba 1:12]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya