The chat will start when you send the first message.
1Basi Isaka akamwita Yakobo, akambariki, akamwagiza akamwambia, Usitwae mke wa binti za Kanaani.[#Mwa 27:33]
2Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.
3Na Mungu Mwenyezi, akubariki, akuzidishe, na kukuongeza, ili uwe mtu wa watu wengi.[#Mwa 17:1,6]
4Akupe baraka ya Abrahamu, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, Mungu aliyompa Abrahamu.[#Mwa 17:4-8; Mwa 12:2; 22:17; 1 Nya 29:15; Zab 39:12; 2 Kor 5:6,7; Ebr 11:9,13; 1 Pet 1:17; 2:11]
5Basi Isaka akamtuma Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.
6Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumtuma Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usioe mke wa binti za Kanaani,
7na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu.
8Esau akaona ya kuwa binti za Kanaani hawakumpendeza Isaka, baba yake.[#Mwa 24:3]
9Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Abrahamu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao.[#Mwa 25:13; 36:3]
10Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani.[#Mdo 7:2]
11Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.
12Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.[#Yn 1:51; Mwa 41:1; Ayu 33:15; Ebr 1:14]
13Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii unayolala nitakupa wewe na uzao wako.[#Mwa 13:14-15; Mwa 35:1; 48:3; 26:24]
14Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.[#Mwa 12:3; 22:18; Mwa 13:14-16; Kum 12:20]
15Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.[#Mwa 26:24; 35:6; 48:16; Zab 121:5; Kum 31:6; Hes 23:19]
16Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, ijapokuwa mimi sikujua.[#Kut 3:5; Yos 5:15]
17Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.
18Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
19Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.[#Amu 1:23; Hos 4:15]
20Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;[#Mwa 28:15; 31:13; Amu 11:30; 2 Sam 15:8; 1 Tim 6:8]
21nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.[#Amu 11:31; 2 Sam 15:8; 19:24; Kum 26:17; 2 Fal 5:17]
22Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.[#Mwa 35:7; Law 27:30]