The chat will start when you send the first message.
1Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.[#2 Fal 4:8]
2Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake.[#Mwa 34:2; 1 Nya 2:3]
3Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.[#Hes 26:19]
4Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.[#Mwa 46:12]
5Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwa huko Kezibu, alipomzaa.[#Hes 26:20]
6Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.[#Mwa 24:4]
7Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua.[#Mwa 46:12; 1 Nya 2:3]
8Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.[#Mt 22:24]
9Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, alimwaga mbegu chini asimpe nduguye uzao.[#Kum 25:6]
10Jambo hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye pia.[#Hes 26:19]
11Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.[#Rut 1:13; Law 22:13]
12Siku nyingi zikapita, akafa binti Shua, mkewe Yuda. Yuda akafarijika, akaenda kwa watu wake wawakatao kondoo manyoya huko Timna, yeye na mwenzake Hira, Mwadulami.[#2 Sam 13:39]
13Huyo Tamari akapewa habari, kusema, Mkweo anakwenda Timna, akate manyoya ya kondoo wake.[#Yos 15:10,57]
14Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.[#Mit 7:12; Mwa 38:11,26]
15Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.
16Akamgeukia kando ya njia, akasema, Niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, Utanipa nini, ukiingia kwangu?
17Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi kutoka kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta?[#Eze 16:33]
18Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya mhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba.[#Mwa 38:25]
19Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake.[#Mwa 38:14]
20Yuda akapeleka yule mwana-mbuzi kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami, ili aipate rehani mkononi mwa huyo mwanamke lakini hakumkuta.
21Akauliza watu wa mji ule, akisema, Yuko wapi yule kahaba aliyekuwapo Enaimu kando ya njia? Wakasema, Hakuwako hapa kahaba.
22Akamrudia Yuda akasema, Sikumwona; hata na watu wa mahali hapo walisema, Hakuwako kahaba.
23Yuda akasema, Na aichukue yeye, tusije tukatiwa aibu; tazama, nimempelekea mbuzi huyu, wala hukumkuta.
24Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mke wa mwana wako, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.[#Amu 19:2; Law 21:9; Kum 22:21]
25Alipotolewa, alituma watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii.[#Mwa 37:32]
26Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.[#1 Sam 24:17; Mwa 38:14; Ayu 34:31]
27Ikawa, wakati wake wa kuzaa walikuwapo mapacha tumboni mwake.
28Ikawa alipokuwa akizaa, mtoto mmoja akatoa mkono, mkunga akautwaa uzi mwekundu akaufunga mkononi mwake, huku akisema, Huyu ametoka kwanza.
29Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka. Akasema, Mbona umepita kwa nguvu wewe? Mambo ya nguvu na yakuandame. Kwa hiyo jina lake likaitwa Peresi[#38:29 Peresi: maana yake ni ‘kutoka kwa nguvu’.]
30Akatoka ndugu yake baadaye, ana uzi mwekundu mkononi mwake; naye akaitwa jina lake Zera.[#38:30 Zera maana yake ni ‘enye kung'aa’.]