The chat will start when you send the first message.
1Na katika siku hiyo utasema,[#Isa 2:11; Zek 14:20,21]
Ee BWANA, nitakushukuru wewe;
Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia,
Hasira yako imegeukia mbali,
Nawe unanifariji moyo.
2Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;[#Kut 15:2; Zab 118:14]
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
3Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.[#Yer 2:13; Yn 4:10,14]
4Na katika siku hiyo mtasema,
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.
5Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
6Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;[#Isa 54:1; Sef 3:14; Lk 19:37-40]
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.