The chat will start when you send the first message.
1Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.[#Eze 29:3; Ayu 41:1; Zab 74:14; 104:26]
2Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.
3Mimi, BWANA, nililinda,
Nitalitia maji kila dakika,
Asije mtu akaliharibu;
Usiku na mchana nitalilinda.
4Mimi sina hasira ndani yangu;[#2 Sam 23:6]
Kama mbigili na miiba ingekuwa mbele zangu,
Ningepanga vita juu yake,
Ningeiteketeza yote pamoja.
5Au azishike nguvu zangu,[#Ayu 22:21; Isa 53:4,5; Efe 2:12-14]
Afanye amani nami;
Naam, afanye amani nami.
6Siku zijazo Yakobo atatia mizizi;[#Isa 37:31; Hos 14:5,6]
Israeli atatoa maua na kuchipuka;
Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
7Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?
8Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.[#Ayu 23:6; Zab 6:1; Yer 10:24; 1 Kor 10:13]
9Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
10Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake.[#Isa 17:2]
11Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.[#Kum 32:18,28; Zab 28:5; Isa 1:3; 44:2,21,24; Yer 4:22; 2 The 1:8]
12Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA atayapigapiga matunda yake toka gharika ya Mto hadi kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
13Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.[#Isa 2:11; Hes 10:2; Zab 81:3; Hos 8:1; Mt 24:31; Ufu 11:15]