The chat will start when you send the first message.
1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
2Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA.[#Isa 65:15; Ufu 3:12]
3Nawe utakuwa taji la uzuri katika mkono wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.[#Zek 9:16]
4Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.[#Hos 1:10; 1 Pet 2:10; #62:4 maana yake ni ‘namfurahia.’; #62:4 maana yake ni ‘ameolewa.’]
5Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.
6Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;[#Wim 3:3; Isa 52:8; Eze 3:17; Ebr 13:17]
7wala msimwache akae kimya, mpaka atakapouimarisha Yerusalemu, na kuufanya usifike kote duniani.[#Isa 61:11; Sef 3:20]
8BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.[#Kum 28:31; Yer 5:17]
9Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.[#Kum 12:12]
10Piteni, piteni, katika malango;
Itengenezeni njia ya watu;
Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;
Twekeni bendera kwa ajili ya makabila ya watu.
11Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia,[#Zek 9:9; Mt 21:5; Yn 12:15; Isa 40:10; 49:4; Ufu 22:12]
Mwambieni binti Sayuni,
Tazama, wokovu wako unakuja;
Tazama, thawabu yake iko pamoja naye,
Na malipo yake yako mbele zake.
12Nao watawaita, Watu watakatifu,
Waliokombolewa na BWANA;
Nawe utaitwa, Aliyetafutwa,
Mji usioachwa.