The chat will start when you send the first message.
1Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, akiwa katika tumbo la yule samaki,
2Akasema,
Nilimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu,
Naye akaniitikia;
Katika tumbo la kuzimu niliomba,
Nawe ukasikia sauti yangu.
3Maana ulinitupa vilindini,[#Zab 88:6]
Ndani ya moyo wa bahari;
Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;
Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
4Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;[#Zab 31:22; Isa 49:14; 1 Fal 8:38]
Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
5Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;
Vilindi vilinizunguka;
Mwani ulikizinga kichwa changu;
6Nilishuka hata pande za chini za milima;
Hiyo nchi ambayo mapingo yake yanafunga hata milele;
Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka humo shimoni,
Ee BWANA, Mungu wangu,
7Roho yangu ilipozimia ndani yangu,[#Zab 18:6; 34:6; 130:2; Yer 2:13]
Nilimkumbuka BWANA;
Maombi yangu yakakufikia,
Katika hekalu lako takatifu.
8Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo[#2 Fal 17:15; Zab 31:6; Yer 10:8]
Hujitenga na rehema zao wenyewe.
9Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;[#Zab 50:14; 66:13-15; Hos 14:2; Ebr 13:15]
Nitaziondoa nadhiri zangu.
Wokovu hutoka kwa BWANA.
10BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.[#Yon 1:17; Mt 8:9]