The chat will start when you send the first message.
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2Hii ndiyo sheria ya mwenye ukoma, katika siku ya kutakaswa kwake; ataletwa kwa kuhani,[#Mt 8:2,4; Mk 1:40,44; Lk 5:12,14; 17:14; Yer 15:19; Eze 44:23]
3na huyo kuhani atatoka aende nje ya kambi; na kuhani ataangalia, ikiwa pigo la ukoma limepoa kwake huyo mwenye ukoma;
4ndipo huyo kuhani ataagiza kwamba watwae kwa ajili yake atakayetakaswa ndege wawili walio hai, ambao ni safi, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo;[#Hes 19:6; Ebr 9:19; Kut 12:22; Hes 19:18; Zab 51:7]
5kisha kuhani ataagiza ndege mmoja achinjwe katika chombo cha udongo kilicho juu ya maji ya mtoni;
6kisha huyo ndege aliye hai atamshika, na huo mti wa mwerezi, na hiyo sufu nyekundu, na hisopo, naye atavichovya, pamoja na yule ndege aliye hai, katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa juu ya maji ya mtoni;
7kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba ni safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani.[#Eze 36:25; Ebr 9:13; 10:22; Law 8:11; 2 Fal 5:10,14]
8Naye huyo atakayetakaswa atazifua nguo zake, na kunyoa nywele zake zote, na kuoga katika maji, naye atakuwa safi; baada ya hayo ataingia ndani ya kambi, lakini ataketi nje ya hema yake muda wa siku saba.[#Law 13:6; 11:25; Hes 5:2,3; 12:14,15; 2 Nya 26:20,21]
9Kisha siku ya saba atanyoa nywele zote za kichwani mwake, na ndevu zake, na nyusi zake, nywele zake zote pia atazinyoa; kisha atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa safi.
10Kisha siku ya nane atachukua wana-kondoo wawili wa kiume wasio na dosari, na mwana-kondoo mmoja wa kike wa mwaka wa kwanza asiye na dosari, na sehemu tatu za kumi za efa moja ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, kuchanganywa na mafuta, na logi moja ya mafuta.[#Mt 8:4; Mk 1:44; Lk 5:14; Law 2:1; Hes 15:4; #14:10 Kipimo cha kilo tatu.; #14:10 Kipimo cha vitu viowevu kinachotoshana na theluthi moja ya lita.]
11Kisha kuhani atakayemtakasa atamsimamisha huyo mtu atakayetakaswa, pamoja na vitu vile vyote, mbele za BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania;
12kisha kuhani atamshika mmoja kati ya hao wana-kondoo wa kiume, na kumsongeza awe sadaka ya hatia, pamoja na hiyo logi ya mafuta, kisha atavitikisa kuwa ni sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA;[#Law 5:2-6; 6:6,7; Kut 29:24]
13kisha atamchinja huyo mwana-kondoo mahali hapo wachinjiapo sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, ndani ya mahali patakatifu; kwa kuwa kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo ya kuhani, ndivyo ilivyo sadaka ya hatia; ni takatifu sana;[#Isa 53:7; Yn 1:29; 1 Pet 1:19; Ufu 5:6; Kut 29:11; Law 1:5,11; 7:7; 2:3; 7:6]
14kisha huyo kuhani atatwaa baadhi ya hiyo damu ya sadaka ya hatia, naye kuhani ataitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;[#Efe 1:7; Kol 1:14; Ebr 9:9-14; Ufu 12:11; Kut 29:20; Law 8:23; Rum 12:1; 2 Kor 7:1]
15kisha kuhani atatwaa katika hiyo logi ya mafuta, na kuyamimina katika kitanga cha mkono wake mwenyewe wa kushoto;
16kisha kuhani atatia kidole cha mkono wa kulia katika hayo mafuta, yaliyo katika mkono wake wa kushoto, naye atayanyunyiza hayo mafuta kwa kidole chake mara saba mbele za BWANA;
17na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani atayatia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya damu ya sadaka ya hatia;[#Rum 6:13-22; 12:1; 1 Kor 6:20]
18na mafuta yaliyobaki, yaliyo katika mkono wa kuhani, atayatia juu ya kichwa cha huyo atakayetakaswa; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, mbele za BWANA.[#Law 4:26; Hes 15:28; Dan 9:24; Rum 3:23-25; 5:11; 2 Kor 5:18,19; Efe 2:12-22; Kol 1:19-22; Ebr 2:17; 9:9-14; 1 Yoh 1:7; 4:10]
19Kisha kuhani atasongeza sadaka ya dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa kwa sababu ya unajisi wake; kisha baadaye ataichinja sadaka ya kuteketezwa;
20kisha kuhani ataisongeza hiyo sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, juu ya madhabahu na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.
21Lakini akiwa ni maskini, naye hawezi kupata kiasi hicho, ndipo atatwaa mwana-kondoo mmoja wa kiume, awe sadaka ya hatia ya kutikiswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake, na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba, uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga, na logi ya mafuta;[#Law 5:7; 12:8; Ayu 34:19; Mit 17:5; 22:2; Mt 11:30; Lk 6:20; 1 Yoh 5:3]
22na hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kama awezavyo kuwapata; huyo mmoja atakuwa sadaka ya dhambi, na wa pili atakuwa sadaka ya kuteketezwa.[#Law 12:8; 15:14,15; Lk 2:24]
23Hata siku ya nane atawaleta kwa kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania mbele za BWANA, kwa ajili ya kutakaswa kwake.
24Na kuhani atamtwaa huyo mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na hiyo logi ya mafuta, naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA;
25kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;[#1 The 5:23; 1 Yoh 1:7; Ufu 1:5; 7:14]
26kisha kuhani atajimiminia baadhi ya mafuta hayo katika kitanga cha mkono wake wa kushoto;
27kisha kuhani atanyunyiza baadhi ya hayo mafuta yaliyo katika mkono wake wa kushoto, kwa kidole chake cha mkono wa kulia mara saba mbele za BWANA;
28kisha kuhani atatia mengine katika hayo mafuta yaliyo mkononi mwake katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya mahali pale penye damu ya sadaka ya hatia;[#1 Kor 6:11]
29na mafuta yaliyobaki katika mkono wa kuhani atayatia juu ya kichwa cha huyo atakayetakaswa, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA.
30Kisha atasongeza hao hua mmojawapo, au hao makinda ya njiwa mmojawapo, kadiri ya awezao kuwapata;[#Law 15:15; Rum 8:3]
31hata kadiri aliyoweza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya unga; na huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake huyo atakayetakaswa mbele za BWANA.
32Huyo ambaye ndani yake mna pigo la ukoma, ambaye hawezi kukipata hicho kipasacho kutakaswa kwake, sheria yake ni hiyo.
33BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
34Hapo mtakapoingia nchi ya Kanaani, ambayo nawapa kuwa ni milki yenu, nami nitakapolitia pigo la ukoma katika nyumba ya nchi hiyo ya milki yenu;[#Mwa 17:8; Hes 32:22; Kum 7:1; 19:1; 32:39; Isa 45:7; Amo 3:6; Mik 6:9]
35ndipo mwenye nyumba hiyo atakwenda na kumwambia kuhani, akisema, Naona mimi ya kwamba pana kama pigo katika nyumba yangu;[#Zab 91:10; Mit 3:33; Zek 5:4]
36ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, kabla kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili vyote vilivyomo nyumbani visiwe najisi, kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aikague;[#Hes 19:18; Zab 51:7; Isa 52:11; 1 Kor 5:6,7; 15:33; 2 Kor 6:17; 2 The 3:6; 1 Tim 5:22; Ufu 18:4]
37naye ataliangalia hilo pigo, na tazama, likiwa pigo limo ndani ya kuta za nyumba, nalo lina mashimo-mashimo, rangi ya majani, au mekundu, na kuonekana kuingia ndani kuliko huo ukuta;
38ndipo kuhani atatoka katika nyumba hiyo mpaka mlangoni pa nyumba, na kuifunga hiyo nyumba muda wa siku saba;
39siku ya saba kuhani atakwenda tena, naye ataangalia; na tazama, likiwa pigo limeenea katika kuta za nyumba;
40ndipo kuhani atawaambia wayatoe hayo mawe, yaliyo na pigo, na kuyatupa mahali penye uchafu nje ya mji;[#Yer 15:19; Eze 22:26; 44:23]
41naye atafanya kwamba hiyo nyumba ikwanguliwe ndani pande zote, na chokaa watakayokwangua wataimwaga nje ya mji mahali palipo na uchafu;
42kisha watatwaa mawe mengine, na kuyatia mahali pa mawe hayo; naye atatwaa chokaa nyingine, na kuipaka chokaa hiyo nyumba.
43Na kama hilo pigo likirudi tena, na kutokea ndani ya nyumba, baada ya yeye kuyatoa hayo mawe, na baada ya kuikwangua nyumba, na baada ya kupakwa chokaa,
44ndipo kuhani ataingia ndani na kuangalia, likiwa pigo limeenea ndani ya hiyo nyumba, ni ukoma unaodhuru hiyo nyumba; ni unajisi.[#Law 13:51; Zek 5:4]
45Naye ataibomoa nyumba, mawe yake, na miti yake, na chokaa yote ya hiyo nyumba; naye atavichukua vyote nje ya mji hadi mahali palipo na uchafu.
46Tena mtu atakayeingia ndani ya hiyo nyumba wakati huo wote iliofungwa, atakuwa najisi hadi jioni.[#Law 17:15; 22:6; Hes 19:7-10,21,22; 1 Kor 15:33]
47Na mtu alalaye ndani ya nyumba hiyo atazifua nguo zake, naye alaye chakula ndani ya nyumba hiyo atazifua nguo zake.
48Kisha kuhani akiingia ndani kukagua na kuona kuwa pigo halikuenea katika hiyo nyumba baada ya nyumba kupakwa chokaa; ndipo kuhani atatangaza kuwa nyumba hiyo ni safi, maana pigo limepoa.[#Kum 32:39; Ayu 5:18; Hos 6:1; Mk 5:29; Lk 7:21]
49Naye atatwaa ndege wawili, na mti wa mwerezi, na sufu nyekundu, na hisopo, kwa kuitakasa hiyo nyumba;
50naye atamchinja mmojawapo wa ndege hao katika chombo cha udongo kilicho juu ya maji ya mtoni;
51kisha atatwaa huo mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, pamoja na huyo ndege aliye hai, na kuvichovya vyote katika damu ya huyo ndege aliyechinjwa, na katika hayo maji ya mtoni, na kuinyunyizia nyumba mara saba;[#1 Fal 4:33; Zab 51:7]
52naye ataitakasa hiyo nyumba kwa damu ya ndege, na kwa maji ya mtoni, na kwa huyo ndege aliye hai, na kwa mti wa mwerezi, na kwa hisopo, na kwa sufu nyekundu;
53lakini ndege aliye hai atamwacha atoke mle mjini aende nyikani; ndivyo atakavyofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo nyumba; nayo itakuwa safi.
54Hiyo ndiyo sheria ya pigo la ukoma ya kila aina, na ya kipwepwe;[#Law 13:30]
55na ya ukoma wa vazi, na ukoma wa nyumba;[#Law 13:47]
56na kivimbe, na kikoko na kipaku king'aacho;[#Law 13:2]
57ili kufunza itakapokuwa ni unajisi, na itakapokuwa ni safi; hiyo ndiyo sheria ya ukoma.[#Kut 15:26; Kum 4:6; 24:8; Zab 78:5; 119:96; Mit 6:23; Eze 44:23]