The chat will start when you send the first message.
1Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa mtawala wa Yudea, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,
2wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.
3Akafika katika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba iletayo ondoleo la dhambi,[#Mt 3:1-12; Mk 1:1-8]
4kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya nabii Isaya;[#Isa 40:3-5]
Sauti ya mtu aliaye nyikani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Yanyosheni mapito yake.
5Kila bonde litajazwa,
Na kila mlima na kilima kitashushwa;
Palipopindika patakuwa pamenyoka,
Na palipoparuza patalainishwa;
6Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.[#Mdo 28:28]
7Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazawa wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?[#Mt 12:34; 23:33; Yn 3:36]
8Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Abrahamu watoto.[#Yn 8:33]
9Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa kwenye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.[#Mt 7:19]
10Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi?
11Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo.
12Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi?[#Lk 7:29]
13Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa.
14Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
15Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza mioyoni mwao kuhusu Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo,[#Yn 1:19-28]
16Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza kamba ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto;[#Mdo 13:25]
17ambaye ungo wake uko mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanja wake wa kupuria, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
18Basi, kwa maonyo mengine mengi aliwahubiria watu.
19Lakini mfalme Herode alipokaripiwa na yeye kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, na maovu yote aliyoyafanya Herode,[#Mt 14:3-4; Mk 6:17-18]
20aliongeza na hili juu ya yote, alimfunga Yohana gerezani.
21Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;[#Mt 3:13-17; Mk 1:9-11; Yn 1:32]
22Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.[#Mwa 22:2; Zab 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; Mk 1:11; Lk 9:35]
23Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri wa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,[#Mt 1:1-17; #Lk 4:22]
24wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu,
25wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai,
26wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda,
27wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri,[#1 Nya 3:17; Ezr 3:2]
28wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri,
29wa Yoshua, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi,
30wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu,
31wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi,[#1 Sam 16:1,13; 2 Sam 5:14]
32wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni,[#Rut 4:22]
33wa Aminadabu, wa Admini, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda,[#1 Nya 2:1-5; Mwa 29:35]
34wa Yakobo, wa Isaka, wa Abrahamu, wa Tera, wa Nahori,[#Mwa 21:2,3; 11:10-26; 1 Nya 1:24-27]
35wa Serugi, wa Regau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala,
36wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki,[#Mwa 5:3-32; 1 Nya 1:1-4; Mwa 4:25; 11:10]
37wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani,
38wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.[#Mwa 5:1-3]