The chat will start when you send the first message.
1Basi sasa, sikieni asemavyo BWANA; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako.
2Sikieni, enyi milima, shutuma ya BWANA, na ninyi, enyi misingi ya dunia iliyo imara; kwa maana BWANA ana shutuma na watu wake, naye atahojiana na Israeli.[#Hos 12:2]
3Enyi watu wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa kitu gani? Shuhudieni juu yangu.[#Zab 50:7; Isa 5:3,4; Yer 2:5,31]
4Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.[#Kut 4:10-16; 12:50-51; 15:20]
5Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni yaliyotukia toka Shitimu hadi Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.[#Ufu 2:14; Hes 25:1; Amu 5:11; Hes 22:2—24:25; Yos 3:1—4:19]
6Nimwendee BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimwendee na sadaka za kuteketezwa, na ndama wa umri wa mwaka mmoja?[#Zab 15:1; Yn 6:28]
7Je! BWANA atapendezwa na maelfu ya kondoo dume, au na makumi elfu ya mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzawa wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?[#Zab 50:9; Isa 1:11; 2 Fal 16:3]
8Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!
9Sauti ya BWANA inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.
10Je! Hata sasa hazina za uovu zingalimo nyumbani mwa wabaya, na kipimo kilichopunguka, ambacho ni chukizo?
11Je! Naweza kuwa safi nami nina mizani ya udhalimu, na mfuko wa mawe ya kupimia ya udanganyifu?[#Hos 12:7; Amo 3:10]
12Kwa maana matajiri wake wamejaa jeuri, na wenyeji wake wamesema uongo, na ulimi wao una udanganyifu kichwani mwao.
13Basi, kwa ajili ya hayo, mimi nami nimekupiga kwa pigo liumizalo sana; nimekufanya kuwa ukiwa, kwa sababu ya dhambi zako.
14Utakula, lakini hutashiba; ndani yenu njaa itazidi kuwauma; nawe utahama, lakini hutachukua kitu salama; na hicho utakachochukua nitakitoa kwa upanga.
15Utapanda, lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka mafuta; na hizo zabibu, lakini hutakunywa divai.
16Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.[#1 Fal 16:23-34; 21:25-26]