The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,
Nitaimba, nitaimba zaburi,
Naam, kwa utukufu wangu.
2Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
3Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia sifa kati ya mataifa.
4Maana fadhili zako ni kubwa kuliko mbingu,[#Mik 7:18-20; Hes 14:18; Kum 7:9; Zab 36:5]
Na uaminifu wako unafika hata mawinguni.
5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,[#Zab 57:5]
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6Ili watu uwapendao waokolewe,
2 Unipe ushindi kwa mkono wako wa kulia, na uniitikie.
7Mungu amenena kwa utakatifu wake,
Nami nitashangilia.
Nitaigawanya Shekemu,
Nitalipima bonde la Sukothi.
8Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,[#Mwa 49:10; Zab 60:7]
Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.
Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,
9Moabu ni bakuli langu la kunawia.
Nitamtupia Edomu kiatu changu,
Na kumpigia Filisti kelele za vita.
10Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma?[#Zab 60:9]
Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu?
11Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?
Wala, Ee Mungu, huendi na majeshi yetu?
12Utuletee msaada juu ya mtesi,
Maana wokovu wa binadamu haufai.
13Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,[#Isa 25:10; 30:3; Omb 1:15; Mal 4:3; Mdo 1:20; Ufu 14:19-20]
Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.