The chat will start when you send the first message.
1Nayainua macho yangu niitazame milima,
Msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu hutoka kwa BWANA,
Aliyezifanya mbingu na nchi.
3Hatauacha mguu wako usogezwe;[#1 Sam 2:9; Isa 27:3]
Akulindaye hatasinzia;
4Naam, hatasinzia wala hatalala,
Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5BWANA ndiye mlinzi wako;
BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.
6Jua halitakupiga mchana,[#Isa 49:10]
Wala mwezi wakati wa usiku.
7BWANA atakulinda na mabaya yote,[#Ayu 5:19; Zab 91:9,10; Mit 12:21]
Atakulinda nafsi yako.
8BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,[#Kum 28:6; Mit 2:8]
Tangu sasa na hata milele.