The chat will start when you send the first message.
1Nilifurahi waliponiambia,[#Isa 2:3; Yer 31:6; Zek 8:21]
Twende nyumbani kwa BWANA.
2Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
3Ee Yerusalemu uliyejengwa[#2 Sam 5:9; Efe 2:21]
Kama mji ulioshikamana,
4Huko ndiko wapandako kabila,[#Kum 16:16; Kut 16:34]
makabila ya BWANA;
Kama ulivyowaamuru Waisraeli,
Walishukuru jina la BWANA.
5Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya ukoo wa Daudi.
6Uombeeni Yerusalemu amani;[#Isa 62:6; Yer 51:50]
Na wafanikiwe wakupendao;
7Amani na ikae ndani ya kuta zako,
Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu
Niseme sasa, Amani ikae nawe.
9Kwa ajili ya nyumba ya BWANA, Mungu wetu,
Nitakuombea mema.