Zaburi 123

Zaburi 123

Ombi la huruma

1Nimekuinulia macho yangu,

Wewe uketiye mbinguni.

2Kama vile macho ya watumishi

Yanavyoutegemea mkono wa bwana zao

Kama macho ya mjakazi

Yanavyoutegemea mkono wa bimkubwa wake;

Ndivyo macho yetu yanavyomtegemea BWANA, Mungu wetu,

Hadi atakapoturehemu.

3Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi,

Kwa maana tumeshiba dharau.

4Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha,

Na dharau ya wenye kiburi.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya