The chat will start when you send the first message.
1Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.[#Yer 12:3; Ufu 2:23]
2Wewe wajua kuketi kwangu na kusimama kwangu;[#2 Fal 19:27; Mt 9:4; Yn 2:24]
Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote.
4Maana hamna neno katika ulimini wangu[#Ebr 4:13]
Usilolijua kabisa, BWANA.
5Umenizingira nyuma na mbele,
Ukaniwekea mkono wako.
6Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,
Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.
7Niende wapi nijiepushe na roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
8Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;[#Mit 15:11]
Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9Ningezitwaa mbawa za asubuhi,
Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10Huko nako mkono wako utaniongoza,
Na mkono wako wa kulia utanishika.
11Kama nikisema, Hakika giza litanifunika,
Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;
12Giza nalo halikufichi kitu,
Bali usiku huangaza kama mchana;
Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,
Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
14Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa njia ya ajabu ya kutisha.
Matendo yako ni ya ajabu,
Na nafsi yangu yajua sana,
15Mifupa yangu haikusitirika kwako,
Nilipoumbwa kwa siri,
Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;
16Macho yako yaliniona kabla sijakamilika;
Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia,
Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
17Mawazo yako ni mazito sana kwangu;
Ee Mungu; nayo ni makuu sana.
18Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga;
Niamkapo ningali pamoja nawe.
19Ee Mungu, laiti ungewaua waovu![#Isa 11:4]
Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu;
20Wale wanaokusema kwa ubaya,[#Ayu 21:14,15; Yud 1:15]
na kutenda maovu juu ya jina lako bure.
21Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia?
Nisiudhike nao watu wanaokuasi?
22Nawachukia kwa upepo wa chuki,
Wamekuwa adui kwangu.
23Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu,[#Ayu 31:6]
Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
24Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu,[#Mt 7:14; Yn 14:6]
Ukaniongoze katika njia ya milele.