The chat will start when you send the first message.
1BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,[#2 Sam 15:13—17:22]
Ni wengi wanaonishambulia,
2Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,[#2 Sam 16:8; Zab 22:7,8]
Hana wokovu huyu kwa Mungu.
3Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,[#2 Fal 25:27; Zab 27:6]
Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
4Kwa sauti yangu namwita BWANA
Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.
5Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena,[#Zab 4:8; Mit 3:24; Mdo 12:6]
Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
6Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu,
Waliojipanga Juu yangu pande zote.
7BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,
Maana umewapiga taya adui zangu wote;
Umewavunja meno wasio haki.
8Wokovu ni wa BWANA;[#Zab 37:39,40; Mit 21:31; Hes 13:4]
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.