The chat will start when you send the first message.
1Bwana ndiye aliye mkuu,[#Isa 2:2; Oba 1:17; Mik 4:1]
Na mwenye kusifiwa sana.
Katika mji wa Mungu wetu,
Katika mlima wake mtakatifu.
2Kuinuka kwake ni mzuri sana,[#Mt 5:35; Yer 3:19; Omb 2:15; Eze 20:6; Isa 14:13]
Ni furaha ya dunia yote.
Mlima Sayuni, kule upande wa kaskazini,
Mji wa Mfalme mkuu.
3Mungu katika majumba yake
Amejijulisha kuwa ngome.
4Maana, tazama, wafalme walikusanyika;[#2 Sam 10:6]
Walikuja wote pamoja.
5Mara Walipouona, wakashtuka;
Wakafadhaika na kukimbia.
6Papo hapo tetemeko liliwashika,
Uchungu kama wa mwanamke azaaye.
7Kama upepo wa mashariki[#Eze 27:26]
Unapovunja jahazi za Tarshishi.
8Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona,[#Isa 2:2; Mik 4:1]
Katika mji wa BWANA wa majeshi.
Mji wa Mungu wetu;
Mungu atauimarisha hata milele.
9Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu,
Katikati ya hekalu lako.
10Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu,[#Mal 1:11]
Ndivyo na sifa yako hadi miisho ya dunia.
Mkono wako wa kulia umejaa haki;
11Na ufurahi mlima Sayuni.
Binti za Yuda na washangilie
Kwa sababu ya hukumu zako.
12Tembeeni katika Sayuni,
Uzungukeni mji wote,
Ihesabuni minara yake,
13Tieni moyoni boma zake,
Yafikirini majumba yake,
Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.
14Kwa maana ndivyo alivyo[#Isa 25:9]
MUNGU, Mungu wetu.
Milele na milele
Yeye ndiye atakayetuongoza.