The chat will start when you send the first message.
1BWANA, usinikemee kwa hasira yako,[#Zab 38:1]
Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2BWANA, unifadhili, maana ninanyauka;[#Hos 6:1]
BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3Na nafsi yangu imefadhaika sana;[#Mit 18:14; Mt 26:38]
Na Wewe, BWANA, hadi lini?
4BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5Maana mautini hapana kumbukumbu lako;[#Zab 30:9]
Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6Nimechoka kwa kuugua kwangu;
Kila usiku nakibubujikia kitanda changu;
Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7Macho yangu yameharibika kwa masumbufu,
Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;[#Mt 7:23; Lk 13:27]
Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
9BWANA ameisikia dua yangu;[#Zab 3:4; 31:22; 40:1,2]
BWANA atayatakabali maombi yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
Watarudi nyuma, kwa ghafla wataaibika.