The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, wastahili sifa katika Sayuni,
Na kwako Wewe itaondolewa nadhiri.
2Wewe usikiaye maombi,[#Lk 11:9,10; Isa 66:23]
Wote wenye mwili watakujia.
3Tutakapozidiwa na matendo maovu[#Ebr 9:14]
Wewe utatuondolea uovu wetu.
4Heri mtu yule umchaguaye,[#Zab 33:12]
Na kumkaribisha akae nyuani mwako.
Na tushibe wema wa nyumba yako,
Patakatifu pa hekalu lako.
5Kwa mambo ya kutisha utatujibu,
Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu.
Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia,
Na la bahari iliyo mbali sana,
6Milima waiweka imara kwa nguvu zako,
Huku ukijifunga uweza kama mshipi.
7Watuliza kuvuma kwa bahari,[#Mt 8:26]
Kuvuma kwa mawimbi yake,
Na ghasia za watu;
8Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;[#Ayu 37:5]
Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
9Umeijia nchi na kuisitawisha,
Umeitajirisha sana;
Mto wa Mungu umejaa maji;
Wawapa watu nafaka
Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.
10Matuta yake wayajaza maji;
Wapasawazisha palipoinuka,
Wailainisha nchi kwa manyunyu;
Waibariki mimea yake.
11Umeuvika mwaka taji la wema wako;[#Zab 104:3]
Mapito yako yadondoza unono.
12Huyadondokea malisho ya nyikani,
Na vilima vimejawa na furaha.
13Na malisho yamejawa na kondoo,
Na mabonde yamepambwa nafaka,
Yanashangilia, na kuimba pamoja kwa shangwe.