Zaburi 87

Zaburi 87

Shangwe ya kuishi Sayuni

1Msingi wake upo

Juu ya milima mitakatifu.

2BWANA ayapenda malango ya Sayuni

Kuliko maskani zote za Yakobo.

3Mambo makuu yanasemwa kukuhusu,[#Isa 60:1]

Ee Mji wa Mungu.

4Nitataja Rahabu na Babeli

Miongoni mwao wanaonijua.

Tazama Filistia, na Tiro, na Kushi;

Wanasema, Huyu alizaliwa humo.

5Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa,[#Eze 48:35; Mt 16:18]

Huyu na huyu alizaliwa humo.

Na Yeye Aliye Juu

Atauimarisha.

6BWANA ataweka kumbukumbu, awaandikapo mataifa,[#Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9]

Huyu alizaliwa humo.

7Waimbao na wachezao ngoma na waseme,

Visima vyangu vyote vimo mwako.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya