The chat will start when you send the first message.
1Njoni, tumwimbie BWANA,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
2Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
3Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,
Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4Mkononi mwake zimo bonde za dunia,
Hata vilele vya milima ni vyake.
5Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na mikono yake iliumba nchi kavu.
6Njoni, tuabudu, tusujudu,[#1 Fal 8:54; 1 Nya 6:13; Ezr 9:5; Dan 6:10; Lk 22:41; Mdo 7:60; 1 Kor 6:20; Efe 3:14; Ayu 35:10; Isa 54:5; Yn 1:3]
Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
7Kwa maana ndiye Mungu wetu,[#Ebr 3:7-11,15; 4:7; Zab 95:7-11; Hes 14:22]
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
8Msifanye mioyo yenu kuwa migumu;[#Kut 17:1-7; Hes 20:2-13]
Kama ilivyokuwa huko Meriba
Kama siku ile katika Masa jangwani.
9Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
10Miaka arubaini nilichukizwa na kizazi kile,[#Ebr 3:10]
Nikasema, Hawa ni watu wenye mioyo inayopotoka,
Na wanaopuuza njia zangu.
11Ndipo Nikaapa kwa hasira yangu[#Hes 14:20-23; Kum 1:34-36; 12:9-10; Ebr 4:3,5]
Hawataingia katika pumziko langu.