The chat will start when you send the first message.
1Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.[#Ezr 2:59; Neh 7:5; Law 26:33; 2 Nya 33:11; 36:5]
2Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika hozi zao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.[#Ezr 2:70; Neh 7:73; Yos 9:27; Ezr 2:43; 8:20]
3Na huko Yerusalemu walikuwa wakikaa baadhi ya wana wa Yuda, na wana wa Benyamini, na wana wa Efraimu na Manase;[#Neh 11:1]
4Uthai, mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imli, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.[#Mwa 46:12; Hes 26:20]
5Na wa Washiloni; Asaya, mzaliwa wa kwanza, na wanawe.
6Na wa wana wa Zera; Yeueli, na ndugu zao; watu mia sita na tisini.
7Na wa wana wa Benyamini; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;
8na Ibneya, mwana wa Yerohamu; na Ela, mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu, mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya;
9na ndugu zao, sawasawa na vizazi vyao; watu mia kenda na hamsini na sita. Watu hao wote ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, kwa kadiri ya mbari za baba zao.
10Na katika makuhani; Yedaya, na Yehoyaribu, na Yakini;[#Neh 11:10; 12:19]
11na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;
12na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; na Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yazera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri;
13wakuu wa mbari za baba zao; pamoja na ndugu zao; watu elfu na mia saba na sitini; watu wenye ustadi waliofaa sana kwa kazi ya huduma ya nyumba ya Mungu.
14Na katika Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari;[#1 Nya 6:19; Neh 11:15-19]
15na Bakbakari, na Hereshi, na Galali, na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu;
16na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.[#1 Nya 2:54; Neh 7:26; 12:28]
17Na katika mabawabu; Shalumu, na Akubu, na Talmoni, na Ahimani, na ndugu zao; naye Shalumu alikuwa mkuu wao;[#1 Nya 23:5; 26:1; Zab 84:10]
18ambao tangu hapo walikuwa wakingojea penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa wangojezi wa rago la wana wa Lawi.[#2 Fal 11:19; Eze 44:23]
19Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa mbari ya babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ungojezi wa malango ya maskani; na baba zao walikuwa wamesimamia matuo ya BWANA, wakiyalinda maingilio;[#Hes 26:9,11; 1 Nya 6:33,38]
20naye Finehasi, mwana wa Eleazari, alikuwa mkuu wao hapo zamani, naye BWANA alikuwa pamoja naye.[#Kut 6:25; Hes 3:32; 25:11; 31:6; Yos 22:30,31; Zab 106:30]
21Zekaria, mwana wa Meshelemia, alikuwa bawabu mlangoni pa ile hema ya kukutania.
22Hao wote waliochaguliwa kuwa wangojezi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyoamaniwa.[#1 Nya 26:1,2; 1 Sam 9:9]
23Basi watu hao na wana wao walikuwa na usimamizi wa malango ya nyumba ya BWANA, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.
24Hao wangojezi walikuwapo pande zote nne, kuelekea mashariki, na magharibi, na kaskazini, na kusini.[#1 Nya 26:13-19]
25Na ndugu zao, katika vijiji vyao, wakaamaniwa kuingia kila siku ya saba, zamu kwa zamu, ili kuwa pamoja nao;[#2 Fal 11:5; 2 Nya 23:8]
26kwa maana wale wangojezi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, walikuwa na kazi ya kuamaniwa, tena walikuwa juu ya vyumba na juu ya hazina katika nyumba ya Mungu.
27Nao wakalala kandokando nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa ulinzi wake ulikuwa juu yao, nayo ilikuwa kazi yao kuyafungua malango asubuhi baada ya asubuhi.
28Na baadhi yao walikuwa na ulinzi wa vyombo vya huduma; kwani huingizwa kwa hesabu, na kutolewa kwa hesabu vile vile.
29Na baadhi yao waliamaniwa kuviangalia vyombo vya nyumbani, na vyombo vyote vya Patakatifu; na kuwa juu ya unga safi, na divai, na mafuta, na ubani, na manukato.
30Na baadhi ya wana wa makuhani waliweka tayari machanganyiko ya manukato.[#Kut 30:23; 37:29; Wim 1:3,13; Yer 6:20; Eze 27:19,22; Mk 14:3]
31Naye Matithia, Mlawi mmojawapo, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, Mkora, aliamaniwa kazi ya kuviangalia vitu vile vilivyookwa kaangoni.[#Law 6:21]
32Na baadhi ya ndugu zao, wa wana wa Wakohathi, walikuwa juu ya mikate ile ya Wonyesho, ili kuiandaa kila sabato.[#Kut 40:23; Ebr 9:2,24; Yn 6:32,33]
33Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku.[#1 Nya 6:31; 13:8; 15:16]
34Hao walikuwa wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, katika vizazi vyao vyote, watu wakuu; nao walikuwa wakikaa huko Yerusalemu.
35Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, na jina la mkewe aliitwa Maaka;[#1 Nya 8:29]
36na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni; na Suri, na Kishi, na Baali, na Meri, na Nadabu;
37na Gedori, na Ahio, na Zekaria, na Miklothi.
38Na Miklothi akamzaa Shimea. Hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.
39Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.[#1 Nya 8:33]
40Na mwana wa Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.
41Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea.[#2 Sam 9:12; 1 Nya 8:35; #9:41 Taz. 1 Nyakati 8:35.]
42Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;
43na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli;
44naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli